Thursday, 31 July 2014

Taarifa za usajili:Arturo Vidal kutua Man Utd,Khedira kwenda Arsenal huku Chelsea mbioni kutoa offer kwa Aubameyang.



 muda mfupi hujao Arturo Vidal anatarajiwa kuongea na klabu yake Juventus juu ya kubadili uwamuzi wake na kuweka wazi mpango wake wa kujiunga na Man Utd baada ya tetesi za muda mrefu.

Juventus inajitaidi kupambana kwa hali yeyote kuakikisha mchezaji huyo mwenye asili ya Chilean anabakia katika klabu hiyo lakini wakala wake anaonekana kukubaliana na Man Utd..
Arsenal wakiwa tayari wameshasajili wachezaji wapatao wanne huku wakitalajia muda mfupi kupata huduma ya kiungo mkabaji wa Real Madrid Sami Khedira kutua Emarates.

 Madrid wapo tayari kumuuza  Khedira kuliko kumuacha klabuni hapo huku mkataba wake ukiwa umebakia mwaka mmoja kumalizika.

Edinson Cavani amekili kwamba kuna uwezekano wa yeye kujiunga na Man Utd ili kufanya uwezekano wa Angel Di Maria kutua katika klabu hiyo ya PSG.


Hata hivyo,striker huyo wa Uruguayan amedai kuwa bado anaitaji kubakia  Paris Saint-Germain msimu hujao.

Huku ikidaiwa kwamba Pierre-Emerick Aubameyang amekataa kupokea offer kutoka kwa Chelsea katika kipindi hiki cha usajili.

Tetesi hizo zinakuja baada ya The Blues kuwa na mpango wa kuuza vifaa vyake ikiwa ni pamoja na  Romelu Lukaku, Demba Ba na Samuel Eto'o kipindi iki cha usajili.

No comments:

Post a Comment