Monday, 14 July 2014

Wananchi Kilimanjaro watakiwa kukazana kielimu

Wananchi wilayani Rombo Mkoani
Kilimanjaro wametakiwa kuzingatia
Elimu na kushirikiana na serikali
katika juhudi za kuboresha Elimu
kwani ndio njia pekee
itakayowakomboa katika wimbi la
umasikini.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa
jimbo la Rombo, Joseph Selasin,
kwenye mkutano ya hadhara wakati
akihutubia wakazi wa Kata za
Mengeni Kitasha na Mahida wilayani
humo Ikiwa ni mwendelezo wa
Ziara yake katika jimbo hilo.
Mbunge huyo amesema kuwa
anatambua kuwa shule nyingi za kata
wilayani humo zinakabiliwa na
changamoto nyingi, ikiwemo
upungufu wa walimu wa masomo ya
sayansi, vifaa vya kufundishia na
nyumba za
walimu nakuitaka jamii kutozibeza
shule hizo kwani zimekua msaada
sana wilayani humo.
Selasini amesema kuwa serikali
ingebadilisha shule moja ya kata kwa
kila Tarafa iwe Chuo cha Ufundi ili
kuwawezesha wanafunzi wanaokosa
fursa ya kuendelea na masomo ya
Sekondari na kidato cha tano
kujifunza
ufundi stadi ili kupunguza wimbi la
vijana wanaokaa vijiweni.

No comments:

Post a Comment