
Bingwa wa Olimpiki na anayeshikilia rekodi ya dunia
katika mbio za mita 800 David Rudisha hakuweza kurudia alichofanya
Glasgow wiki iliyopita katika mbio za mita 800, baada ya kushindwa na
Nigel Amos wa Botswana aliyemaliza wa kwanza kwa dakika moja sekunde
42.45.
Rudisha alimaliza katika nafasi ya tano, licha ya kuongoza mbio hizo kwa muda.
Pierre-Ambroise Bosse wa Ufaransa alimaliza wa pili na Ferguson Rotich Cheruiyot akimaliza wa tatu.
Asbel Kiprop aliyesema atajaribu kuvunja rekodi
ya Hicham El Gerrouj katika mbio za mita 1500, alishindwa kufanya hivyo
na kumaliza nafasi ya pili, baada ya kupitwa na Silas Kiplagat katika
mzunguko wa mwisho.
No comments:
Post a Comment