Sunday, 20 July 2014

Jay Z na Beyonce mbioni kuachana

Ikiwa yamesalia maonyesho 10 ambapo yatafika mpaka septemba mwaka huu mambo yapo tofauti kwa wanandoa hao kutokakana na vyanzo mbalimbali vya habari uko majuu vinaeleza kwamba japokuwa Beyonce na Jay Z wapo kwenye ziara maalumu inayojulikana kama ON THE RUN TOUR  lakini wamelazimika kuwa na mpango maarumu wa kunusulu ndoa yao.
Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na gazeti moja la kila siku The New York Post limeripoti kuwa Jay Z anapaswa kulaumiwa kwa kuvunjika kwa ndoa hiyo kutokana na tabia yake ya kuisaliti ndoa hiyo mara kwa mara japo kuwa ameonekana kufanya kila liwezekanalo ili kulinda mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na kumuajiri mtoa hushauri katika ndoa ambaye atakuwa katika kila safari watakayo kuwa.

No comments:

Post a Comment