Wednesday, 30 July 2014

Yaya Toure sasa kuzeekea Man City

KIUNGO wa mabingwa wa England, Manchester City, Yaya Toure amesema anataka kubakia klabuni hapo kwa muda mrefu kadiri itakavyowezekana.
Nyota huyo mwenye miaka 31 mapema mwaka huu aliripotiwa kutimka Etihad baada ya wakala wake, Dimitri Seluk kusema kuwa Toure alijisikia kutothaminiwa na klabu baada ya kutotumiwa salamu za siku ya kuzaliwa mwezi mei.
Toure mwenye alieleza kuwa anavutiwa kujiunga na matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.
Siku za nyuma Toure alisema kwamba, mashabiki wasisikilize maneno ambayo hayajatoka mdomoni mwake, lakini kila asemacho Dimitri ni sahihi kwasababu anazungumza kwa niaba yake, ingawa kwasasa anasisitiza kuwa wakati wote amekuwa kimya kuhusu furaha yake na hatima yake ya baadaye.

No comments:

Post a Comment