STAR
anayetokea pande za Cameroon Samuel Eto’o ambaye anajulikana sana katika bara
la Afrika kama msakata kabumbu bora kwa muda wote,Eto’o ambaye ametengeneza
jina kupitia ligi aliyokuwa akichezea ya La Liga Spain. Hungana na
mimi katika kukuletea mambo kumi husiyo yajua kuhusu Samuel Eto’o mwanasoka
bora wa muda wote barani Afrika.
Japokuwa Eto’o
hakushiriki kikamilifu katika kombe la dunia lilofanyika Brazili kwa kuwa
alikuwa anauguza maumivu yakifundo cha mguu lakini atabakia kuwa katika
wachezaji bora kuwai kutokea katika ardhi ya Cameroon.
Hata hivyo
bado Eto’o ni mchezaji ambaye anamchango mkubwa katika klabu yake ya Chelsea
ambayo inashiriki katika ligi kuu ya Uingereza ambayo inaushindani mkubwa
balani ulaya.
ETO'O AJULIKANA KAMA “Roger Milla” MDOGO KIPINDI ANACHIPUKIA KISOKA.
Kwa kipaji
alichokuwa nacho kipindi ambacho anaanza kusakata kabumbu wapenzi wa kandanda nchini
Cameroon waka mfananisha na Nguli wa kabumbu Cameroon na barani Afrika wakamwita
“Little Milla”.
Sababu
nyingine za kumwita “Little Milla” pale alipokuwa anapenda kuvaa jezi yenye
jina la Nguli huyo katika mechi alizokuwa akishiriki akiwa mdogo na kulitendea
haki akiwa uwanjani kwa kuonyesha vitu adimu kupelekea kupewa jina hilo.
Moja ya mjadala
uliowahi kutokea BBC kuhusu kipaji cha
Eto’o na kikifananishwa na Roger Milla na kukili kuwa anastaili kubeba jina
hilo kubwa barani Afrika ndipo mmoja wa wachambuzi alisema “Siyo mchezaji bora
Afrika pekee bali alistahili kuwa mmoja
wa wachezaji bora katika mashindano ya kombe la dunia 2006,lakini kati yetu
hatufikilii hilo labda kwakuwa yeye anatokea Afrika.” na kuongeaza kuwa lakini
kupewa jina hilo ni heshima tosha nalinaleta amasa.
ETO'O ALISHAWAI KUKATALIWA KATIKA KLABU ZINAZOFUNDISHA SOKA KWA WATOTO UFARANSA ALIPOKUWA MTOTO.
Kipindi
alipokuwa mototo Eto’o hakuweza kujiunga na klabu zinazofundisha soka Ufaransa
kutokana na tatizo la kitambulisho cha uraia badala yake akatimkia katika klabu
ya watoto ya Real Madrid na kufanikiwa
kuwa moja wanafunzi katika kituo hicho mwaka 1997 na kufanikiwa kucheza kwa
mkopo katika klabu tofauti zinazo cheza katika ligi kuu miaka ya 1990’s.
KWA MARA YA KWANZA AKIWA MCHEZAJI WA KULIPWA ANAFANIKIWA KUPELEKA NYUMBANI KIASI CHA DOLA 200 KATIKA MSHAHALA WAKE WA WIKI.
Kipindi Eto’o
anaanza kulipwa alikuwa pokea zaidi ya dola za kimarekani 200 kwa wiki kitu
ambacho familia yake ilijivunia na katika mahojiano yake alishawai kusema kuwa
Baba yake alishawahi kumuhuliza kuwa” kumbe unaweza kupata pesa nyingi kupitia
mchezo wa mpira?”Eto’o akaongeza kuwa kutokana na amasa hiyo kutoka kwa Baba
yake akajikuta baadae anapesa nyingi kwa kufanya vizuri katika kusakata kabumbu.
HATIMAYE ETO'O ANAMILIKI PASSPORT YA SPAIN AKIWA MCHEZAJI WA KULIPWA.
Baada ya
kusota na kutumia muda mwingi akiwa katika soka la spaini hatimaye Eto’o anafanikiwa kuwa na passport ya
nchi hiyo.
Kitambulishi
hicho “passport”itamuwezesha kutambulika kama sehemu ya Raia wa nchi hiyo na
kumuwezehsa kufanya kazi katika nchi zote zilizopo jumuiya ya ulaya.
June 2007, Eto’o anafunga ndoa na rafiki yake
wa kike wa muda mrefu Georgette na upendelea kwenda kujirusha mara kwa mara
wanapopata muda jijini Paris wakiwa na watoto wao watatu Etienne,Melle na
Siena.
Eto’o anarecord
ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika
kucheza mara nyingi katika ligi kuu ya spain.
Kipindi
kirefu Eto’o ametumia muda wake akichezea ligi ya La liga akiwa mchezaji wa Real Madrid ambapo akitolewa kwa mkopo katika klabu za
Leganes pamoja na Espanyol na nyingine nyingi uwezi kuisahau klabu ya Mallorca
akitumia misimu minne na hatimaye akatua katika viwanja vya nou camp Barcelona
na kufanukiwa kufunga magoli 108 akicheza mara 108.
ETO'O ANATAMBULIKA MCHEZAJI BORA WA MUDA WOTE AFRIKA
Eto’o amefanikiwa
kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2003,2004,2005 na 2010 pia amefanikiwa
kuwa mchezaji bora wa dunia 2005 akiwa nafasi ya tatu katika tuzo zilizotolewa
na FIFA za( runner up for FIFA wourld Player year 2005) kipindi hicho wapenzi
wengi wa mpira walidai Eto’o alistaili kuwa katika nafasi ya kwanza labda
kwa kuwa alikuwa anatokea Afrika.
Ni mmoja ya
washindi wa tuzo ya Gold medal 2000 akiwa na timu yake ya Cameroon katika
mashindano ya Olympic vilevile akiwa na timu yake ya Taaifa ya Cameroon amefanikiwa
kuchukua mara mbili mashindano ya mabingwa wa mataifa ya Afrika.
Eto’o
anajulikana mpachika mabao wa muda wote katika ardhi ya Cameroon na mchezaji wa
tatu kutokea katika Historia ya nchi hiyo.
ETO'O ALISHAWAI KUOGELEA MAJI YA MOTO WAKATI BARCELONA WALIPOSHINDA KOMBE LA LIGA 2004-05
Baada ya
Barcelana kushinda klabu bingwa ulaya 2005 na kupelekea kufanya sherehe katika
uwanja wa Camp Nou huku Eto’o
akiwadhiaki mashabiki wa Mdrid kuwa ni wajinga heshima kwa mabinwa, “Madrid,
carbon, Saluda al campeón”akimaanisha kwa lugha ya kingereza kuwa “Madrid,
bastards, salute the champions.” ambapo kwa kipindi hicho Eto’o alikuwa
Barcelona na pia walikuwa mabingwa ikapelekea uongozi wa klabu yake wamtake
kuomba ladhi kwa Madrid kwa kuwa ndiyo klabu ya kwanza iliyomlea.
ETO'O ALISHAWAI KUANDIKA VITABU NANE JUU YA MAISHA YAKE.
Katika
kitabu chake cha mwisho ambacho
kinasema Bingwa kazaliwa “Birth of
Champion” kinaelezea sana maisha ya key a Utoto tangia akiwa Doula Cameroon.Joel Esso akijulikana katika kitabu hicho ambaye
amevaa uhusika wa Eto’o.
Eto’o
alipotakiwa kueleza sababu za yeye kuandika kitabu hiki alisema kuwa nataka
kutumia lugha ya watoto kwa sababu wao ni kizazi kinachofuata baada ya sisi na
wao pia ni kizazi kinacho tuwakilisha sisi sote pia naitaji kuwasiliana nao kwa
lugha yao.
“Naitaji kutumia
lugha ya watoto kwa kuwa wao ni kizazi kijacho pia wanatuwakilisha sisi sote”alisema
Eto’o katika mahojiano yake.
ETO'O AJENGA SHULE ZA KUKUZA VIPAJI VYA SOKA AFRIKA.
Katika
kusaidia vipaji vya soka Afrika Eto’o akaanzisha Eto’o’s foundation ambayo inahusika
na mipango
Katika Eto’o’o
foundation imefanikiwa kuwa na shule za kukuza vipaji nchini Gabon pamoja na
Nairobi Kenya kama sehemu ya mpango huo huku akisema naitaji kurudisha fadhira kwa
Afrika.
“Nataka
kurudisha shukrani kwa Afrika katika kipindi changu cha kucheza mpira na
kunifanya kuwa bora ”alisema Eto’o

No comments:
Post a Comment