
Mke
wa Kingwendu anayejulikana zaidi kwa jina la mama Maua,
alikutwa na masahibu hayo Alhamisi iliyopita baada ya kuvamiwa
na Upunguvuku anayedaiwa kuwa alikuwa amelewa na kuingizwa
kwenye jumba ambalo halijasha kujengwa lililopo maeneo ya Kwa
Dunga ambapo wapita njia waliwafuma na kuanzisha mtiti…..
Shuhuda
wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe amesema
kuwa, wakati tukio hilo linatokea, Kingwendu mwenyewe alikuwa
safarini na hivyo majirani zake ndio waliomuokoa mkewe……
Hata
hivyo baadhi ya majirani walioongea na mwandishi wamedai kuwa
wawili hao ( Upunguvuku na mama Maua) ni wapenzi wa siku
nyingi na wamekuwa wakionekana mara kadhaa wakienda kunywa
pombe za kienyeji…..
“Huyu
Upunguvuku ni fundi Mwashi, tunamfahamu vizuri kuwa ni hawara
wa mama Maua, mara kadhaa huwa tunawaona wakinywa pombe za
kienyeji pamoja, sema tu leo wamefumwa wakijivinjari ndo
mwanamke anamsingizia eti kambaka,” alisema shuhuda mmoja.
Juhudi
za kumpata Kingwendu kuongelea mkasa huo hazikuzaaa matunda
kutokana na simu yake kutopatikana kila akipigiwa
No comments:
Post a Comment