Monday, 14 July 2014








Takribani  miaka sita sasa toka likabidhiwe kwa mamlaka husika litumike kama  eneo rasmi la biashara lakini bado viongozi wenye dhamana  ya jengo hilo wanasita kuonyesha  nia ya dhati katika kulifanya jengo hilo liwe na tija kwa wafanya biashara wa eneo hilo.
Hali hiyo, inapelekea  wafanya biashara wengi kutokuthamini kuweko kwa jengo hilo na kuona halina  msaada kwao, kutokana na madai ya kuwepo kwa mapungufu makubwa katika maeneo ya jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa miundo mbinu mibovu, kukosekana kwa lift na kutokuweko kwa  kituo cha mabasi ambacho kitasaidia  kuwepo kwa wateja wanao toka maeneo mbalimbali jijini.
Mwenyekiti wa wanyabiashara katika jengo hilo, Abubakari Rakesh, anasema jengo limekosa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ustawi wa wanyabiashara  na kukosekana kwa kituo cha mabasi ambacho kingekuwa chachu ya kupatikana kwa wateja.
“Miundombinu ya jengo si mizuri kwa kukosa vitu muhimu kama vile lift,kituo cha mabasi na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ndio maana utaona wafanyabiashara wengi bado wapo soko la Karume kwakuwa pale kuna kituo cha mabasi na kuna wateja wengi kwa hiyo ni vigumu kuwashawishi kuja eneo amabalo kwao halina tija,” anafafanua Rakeshi
Rakeshi anasema hali hiyo imepelekea kuwaomba halmashauri ya jiji na manispaa ya Ilala iwasaidie katika kutatua kero hizo za muda mrefu kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya jengo lakini mpaka sasa hawajaonesha nia ya dhati katika kutatua madai hayo ambayo yanatoka kwa wafanyabiashara.
Anasema mpaka sasa ni asilimia 30 ambazo zinaonesha muelekeo wa mafanikio ya jengo toka limekabidhiwa kwa mamlaka husika japo kuwa tunapiga hatua katika kushawishi lakini bado zinatakiwa jitihada za makusudi katika kuhakikisha madai ya wafanyabiashara yana sikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa kina.
Katika kukikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazopatikana katika jengo hilo, Rakesh anasema Agosti 31 mwaka jana walikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya Mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala.
“Katika kueleza kamati matatizo yanayotukabili ikiwa pamoja na jengo kukosa lift , kituo cha mabasi,na uwepo kituo cha kuoshea magari mbele ya jengo licha ya kupelekea  usumbufu kwa wateja pia inachangia muonekano mbaya wa jengo, bado mpaka sasa hakuna matokeo yeyote kutoka katika kamati hiyo ambayo yangetoa  ufumbuzi, japokuwa  walituahidi wangetupatia ufumbuzi wa suala hilo mapema,” alisema Rakeshi.
Naye Mwenyekiti Msaidizi, Gerald B.Mpagama,anasema madai ya wafanyabiashara yanagusa  maslahi binafsi ya viongozi walio pewa dhamana,inapelekea  madai hayo yenye msingi kutosikilizwa na kutatuliwa na viongozi hao jambo ambalo linadhohofisha  makusudio na malengo ya serikali katika kufanikisha kuwepo kwa jengo hilo.
“Viongozi wa Halmashauri ya jiji na Manispaa ya Ilala kutokana na maslahi yao binafsi wamekuwa chanzo cha kuwako kwa matatizo haya kwa muda mrefu na kupelekea kudhoofisha kupatikana kwa ufumbuzi wa  matatizo wakati wakijua fika kuwa kuna hasara kubwa inayo patikana kutokana na malengo na makusudio ya kuwepo kwa jengo kutotimia kama ilivyotarajiwa ,”anasema Mpagama.
Mpagama anasema kimsingi Rais Kikwete alitimiza ahadi yake na kulikabidhi jengo tangu 2009, muda wote huo mamlaka husika wameshindwa kusimamia majukumu yao na kusababisha hasara kubwa kutokana na wafanyabiashara wengi bado hawaja shawishika kutokana na kutokuwepo na miundombinu itakayo wavutia wateja.
“Hii sio (mall) kama Mlimani city, kama viongozi wanashindwa kufahamu kuwa pesa nyingi zimetumika kujenga jengo hili na mpaka sasa malengo hayajafikia hata robo,wao baada ya kutatua matatizo hili tufikie malengo,wanadharau na kufikilia ubinafsi na ukiangalia kwa kina Meya wa manispaa ya Ilala (Jeri Slaa) ndio hajafanya  lolote na kashindwa kusimamia kazi yake kwa maslahi ya umma,badala yake yeye anaendeleza  maslahi binafsi, ”alilalamika  Mpagama.
Anasema zipo baadhi ya changamoto zinazo tokana na utoro wa wanyabiashara ambao wanakuwa na vizimba ambavyo hawafanyii biashara bado tunaendelea kufanyia kazi na katika kukabiliana na hilo tumeamua kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara wote wasio na sifa na kuwapa wengine ambao wenye sifa tunazo taka.
“kufungwa kwa vizimba vingi inasababiswa na kuwepo kwa utoro na kupoteza sifa kwa wafanyabiashara wengi wenye vizimba, kutokana na hali hiyo tumeamua  kuchukua vizimba vyote kwa wafanyabiashara walio poteza sifa na wasiokuwa tayari katika maendeleo ya jengo hili  ili tuwapatie wenye sifa za kufanya biashara, ”anafafanua Mpagama.
Katika jitihada za kumtafuta Meya wa jiji la Dar es salaam, Didas Masabuli, ili kujua kwamba ni namna gani ameweza kutafuta ufumbuzi wa  tatizo hilo la muda mrefu, Meya wa jiji alidai kuwa hajui madai hayo na kuelekeza labda mkurugenzi wa jiji angeweza kutambua madai hayo.
“Ningeshauri atafutwe Mgurugenzi wa jiji labda  yeye ndio mwenye data kamili ambazo zitamuezesha kuongelea suala hilo kwa kina,lakini mimi siwezi kuliongelea hilo kwa kuwa hawaku leta madai yao  kwangu , hata hivyo  madai  yao siyatambui  ndio maana nimeshauri  atafutwe mkurugenzi wa jiji ili aliongelee suala hilo, ”anasema Masabuli.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa jiji naye alimtaka mwandishi kumtafuta kiongozi wa jengo kwa kuwa hayuko tayari kulizungumzia suala hilo.
Katika kikao cha kamati (MILADI TAMISEMI), ambacho kilikuwa chini ya mwenyekiti Dk Hamisi kigwangala na waziri Hawa Ghasia, kilichofanyika Agosti 31 mwaka jana mjini Dodoma, kwa mujibu wa mwenyekiti wa wanyabiashara wa Machinga  complex kinaonyesha kuwa baadhi ya viongozi waliokuwepo pamoja na  Meya wa jiji la Dar es salaam Didas Masabuli.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Rakesh, katika kikao na kamati hiyo alipata nafasi ya  kuelezea madai yao mbele ya kamati hiyo pia wakiwemo viongozi  wa jiji na kudai kwamba wange ya shuhulikia madai hayo lakini mpaka sasa hapaja kuwapo matokeo yeyote amabayo yangekuwa ni matokeo mazuri ya kikao hicho.
“Nasikitika sana kwa Meya wa jiji anaposema hayatambui madai yetu, katika kikao ambacho tulikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya mwenyekiti  Dk Hamisi Kigwangala, tukieleza madai yetu nayeye (Didas Masabuli), alikuwapo kwenye  kikao hicho,na haya madai yapo kwa kipindi cha miaka sita sasa,sidhani kama kuna kiongozi mwenye dhamana na hili jengo anaweza kusema hajui madai ya wafanya biashara kama anavyodai yeye (Masaburi), kwamba hayajui madai yetu, ” anasema Rakesh.
Ikumbukwe kwamba jengo hilo lilijengwa kwa mkopo wa NSSF na likakabidhiwa kwa viongozi wa Halmashauri ya jiji  na manispaa ya Ilala miaka sita iliyopita lakini mpaka sasa shughuli katika jengo hilo zimekuwa za kusuasua kutokana na changamoto nyingi katika jengo hilo.

No comments:

Post a Comment