MFUMO mbovu
wa elimu nchini bado ni tatizo kwa shule za msingi na Sekondari katika kuleta
mabadiliko yanayotarajiwa na Sera ya Elimu, matokeo makubwa sasa(BRN), kama
mpango wa wizara unavyo sema.
Ingawa serikali imekuwa
ikibuni mipango mbalimbali ya kuboresha Elimu kama mpango huu wa matokeo
makubwa sasa (BRN) lakini bado ipo haja kwa wizara ya elimu kujitathimini upya ili kufanya
maboresho katika Sera yake kwa kuwa ni tatizo kubwa kwa shule za msingi.
Inaelezwa kuwa
mabadiliko ya mara kwa mara ya Sera ya Elimu yamechangia wanafunzi wengi
kushindwa kusoma na kuandika kutokana na mfumo wa Elimu ulivyo unao mtaka mtoto wa darasa la kwanza asome masomo saba
badala ya matatu.
Tangu Wizara ya Elimu ilipo badilisha Sera ya elimu
inayomtaka mwanafunzi wa darasa la kwanza na darasa la pili kusoma masomo saba badala
ya matatu kama ilivyokuwa mwanzo imepekelekea uelewa mdogo kwa wanafunzi.
Hata hivyo, kinyume na matarajio uamuzi huo haukuweza kuleta matunda mazuri badala
yake umepoteza uwezo wa mtoto wa kusoma na kuandika kwakumpa mtoto mzigo
mkubwa.
Mavuno ya uwamuzi huo
hasi,ndio unafanya leo hii ni jambo la
kawaida kumkuta mtoto wa darasa la saba anamaliza shule hawezi kusoma wala
kuandika kwa ufasaha na inapelekea msingi wake wa elimu kuwa mbovu.
Mwelekeo huo unawatia
hofu wadau mbalimbali wa Elimu nchini wakiwemo walimu , wazazi na wanaharakati
wakidai kuwa mfumo huo wa Elimu bado utaendelea kuzalisha mbumbu wasio jua
kusoma na kuandika kama hautobadilishwa.
Mwalimu Stanley
Muhimbula, ni mwenyekiti wa taaluma katika shule ya msingi Bunge
,anasema kuwa mtoto mdogo inabidi ajifunze kulingana na uwezo wake, unapompa
masomo mengi unamfanya asiweze kuelewa haraka kwa kuwa bado akili yake
inahitaji kukomaa ili aweze kupewa majukumu hayo.
“ Utekelezaji wa (BRN)
ni mgumu sana kulingana na mfumo wa
elimu ulivyo mazingira na baadhi ya mabadiliko ya mfumo unafanya pawe na ugumu
wa watoto kufanya vizuri japo kuwa tunajitahidi sana katika kuwafundisha ila masomo
saba kwa mtoto wa darasa la kwanza bado ni tatizo ,
“Utakuta mtoto wa
darasa la kwanza ana begi kubwa limejaa madaftari na vitabu mpaka utamwonea
uruma anavyo elemewa na hilo begi nabado anafika mpaka darasa la tatu hajui
kusoma kwa ufasaha”anasema Muhimbula
Anasema japokuwa masomo
hayo yameongezwa lakini bado kuna tatizo la walimu katika baadhi ya masomo uku
tukihitajika kualika wageni waje kufundisha somo husika kwa kuwa limekosa
mwalimu wa somo.
“Kuna kompyuta tatu
shule nzima ambayo inawanafunzi wapatao 2000 na izo kompyuta wazazi ndio
wamechangia kuleta na bado kunatatizo la walimu inafikia kipindi inabidi
tuwalike wageni kwa kweli bado kunasari ndefu sana katika kutekeleza matokeo
makubwa sasa(BRN)”anasema Muhumbula
Mwalim anasema wazazi
wanapaswa kuwafatilia watoto wao katika maendeleo ya Elimu na kuakikisha
wanafanya vizuri kwa kuwa mazingira yamebadilika sana,mitando ya kijamii,simu
za mkononi na mfumo wa maisha umebadilika sana sio kama zamani unahitaji mzazi
awe makini kumlinda mtoto.
“Nikweli kuna baadhi ya
watoto sio wasikivu wanacho ambiwa na wazazi lakini suala la kutoa elimu lisiwe
kwa mwalimu bali kila mmoja tuwajibike katika kutoa Elimu ili kuwasaidia hawa
watoto.
“Pia wazazi wasikate tamaa kutokana mazingira
ya sasa ni hatari sana kwa malezi ya mtoto,wanapaswa kuwakumbusha wajibu wao
mara kwa mara bila ya kuchoka ili kumfanya mtoto akue kwenye madili mazuri”anasema
Muhumbula
Naye Mwalim Mkuu Msaidizi
Christina Wambura anaongeza kusema mlundikano wa wanafunzi katika darasa moja
unampa shida mwalim katika kutimiza majukumu ya kuakikisha kila mwanafunzi
anaelewa anachofundishwa.
“ Utakuta darasa lina
wanafunzi 60 mpaka 70 badala ya 45 idadi inayotakiwa,kwetu imechangiwa na
kuwepo kwa shule moja ndani ya kata yetu ambapo utakuta wanafunzi wengi
wanatoka mbali kama vile gongo la mboto,kigamboni na pugu na kusababisha
kupokea wanafunzi wengi tafauti na idadi”anasema
Anasema bado kuna
tatizo kwenye upande wa masomo kama Tehama ambalo linahitaji kuwa na walimu wenye
ufahamu wa somo hilo linalo hitaji kujua Technolojia.
“Bado somo la Tehama
linatoa changamoto kubwa kwa kuwa hakuna walimu wenye ujuzi inafika wakati
inatubidi kuarika mgeni ili wanafunzi wasome”anasema Wambura
No comments:
Post a Comment