Mwanamuziki ambaye ni zao la Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’ Estalina Sanga
‘Linah’ ameaga rasmi jumba hilo ambapo inadaiwa kwa sasa atakuwa chini ya
Kampuni ya No Fake Zone ‘NFZ’ inayoendesha shughuli zake nchini Afrika Kusini.
Taarifa iliyotolewa na aliyewahi kushiriki Shindano
la Big Brother Africa 2003ambaye ndiye msemaji wa kampuni hiyo, Abergail Brigette Plaatjies ‘Abby’ alisema
wamemchukuwa Linah ili kuendeleza kipaji chake kimataifa.
“THT imemlea vizuri Linah na kumfikisha hapa
alipo sasa sisi kama NFZ tumemchukua ili tuweze kumuingiza zaidi kwenye soko la
kimataifa na kwa kuanzia tumeanza kumtengenezea video ya wimbo wake mpya
unaojulikana kwa jina la Oleh Tembah,” alisema Abby
No comments:
Post a Comment