
Zaidi ya watu 2000 wameuawa mwaka huu katika ghasia zilizosababishwa na wapiganaji wa Boko haram.
Huku umwagikaji wa damu ukiendelea Kazkazini mwa Nigeria ,rais Goodluck Johanathan anaendelea kupata shinikizo.
Kuna ripoti kwamba wanajeshi wengi katika vita vya kukabiliana na wanamgambo hao hawana vifaa vya kutosha na hivyo basi kushindwa kuwakabili waasi hao.
Ijapokuwa jeshi halijakiri kuhusu madai hayo linakubali kwamba linahitaji vifaa zaidi ili kukabiliana na vita hivyo.
Rais Goodluck Johnathan anasema kuwa kuna umuhimu wa kulinunulia jeshi vifaa zaidi ili kukabiliana na tishio la Boko Haram.
Wakosoaji hatahivyo wamelishtumu jeshi kwa matumizi mbaya wa raslimali zilizopo.
No comments:
Post a Comment