Pendekezo la kuweka chini silaha
lililotolewa na Misri na kukubaliwa na Israel haliheshimiwi.Jeshi la Israel
limeanza upya kuhujumu vituo vya wapalastina huko Gaza kufuatia kuendelea
kufyetuliwa makombora ya Hamas dhidi ya Israel.Muda mfupi kabla ya hapo baraza
la usalama la Israel liliunga mkono pendekezo hilo.Tawi la kijeshi la Hamas limelipinga
pendekezo hilo lakini afisa mmoja wa tawi la kisiasa alisema
tunanukuu:"Hakuna aliyezungumza na sisi.Pendekezo tumelisikia kupitia
vyombo vya habari.Tunashukuru kwa juhudi zinazofanywa.Lakini tunataka
kuzungumza ana kwa ana na Misri.Tukae na kushauriana na baadae tutatoa jibu
letu kwa pendekezo hilo na marekebisho ya aina gani tunayahitaji."
Waziri mkuu wa Israel alisema hapo
awali makombora ya Hamas yakiendelea kufyatuliwa dhidi ya Israel,basi hujuma za
madage ya kivita ya nchi yake zitazidi makali.Matamshi hayo aliyatoa Netanyahu
wakati wa mkutano na waandishi habari pamoja na waziri wa mambo ya nchi za nje
wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier
No comments:
Post a Comment