Saturday, 26 July 2014

MOURINHO:Wamebugi hatuwezi kutumia pesa za klabu ovyo kama wao kwa kulipa asiye staili................




Chelsea ambao walitaka kumsajili  Luke Shaw dirisha dogo la  January lakini hawakufanikiwa baada ya kugundua angewaghalimu pesa nyingi.
Badala yake  Louis Van Gaal akamkalibisha Manchester United kwa pouni 27m akiwa ni kinda la miaka19 akiwa mchezaji wa timu ya Taifa la uingereza analipwa mshahara wa pouni 100,000 kwa wiki.
Mourinho badala yake akafanikiwa kumsajili mchezaji wa kimataifa mwenye asili ya Brazir Filipe Luis, 28,kwa kiasi kidogo cha mshaala ambao alikuwa akilipwa awali huku kocha uyo akikili kuwa kama angemsajili Shaw kwa kiasi ambacho kilikuwa mezani Pouni 50m basi angebadili hali ya hewa  katika chumba cha kubadilishia nguo cha Chelsea au klabu ingekumbwa na lungu la matumizi mabaya pesa.
“Kama tungemlipa chipukizi wa miaka 19 kama tulivyotakiwa kufanya kwa Luke Shaw tungekuwa kufa.
 “Tungejiua wenyewe katika matumizi mabaya na hali katika vyumba vya kubadilishia nguo ingekuwa mbaya sana”alisema Mourinho.
Alisema endapo utamlipa chipukiza pesa nyingi mwenye kiwango bora, ni sawa, lakini kwa kiwango hicho itakuwaje kwa siku zijazo? Kwa kuwa kunachipukizi ambao kila kukicha vipaji vyao vinaibuka.
‘’Kama utamlipa pesa nyingi kinda wa miaka 19 akiwa ni mchezaji mzuri ni sawa,lakini kama utaendelea kwa mtindo huo kwa wachezaji makinda itakuwaje baadae kwa kuwa  kunachipukizi wengi ambao vipaji vyao vinaibuka.”alisema Mourinho.
 .“Watasema kuwa,Itawezekana vipi?nimekuwa katika klabu hii zaidi  na kufanikiwa kucheza zaidi ya mechi 200 na kushinda makombe kibao,itawezekana vipi kinda la miaka 19 aje hapa apate pesa zaidi  yangu,?
Alisema kuwa kama  hali hiyo itaruhusiwa katika klabu hiyo inaweza kupelekea uchumi wa klabu kupolomoka.
‘’Unaweza kusema Filipe hana thamani ,huku wapenzi  wa  mpira Brazir wanampenda Filipe acheze katika kikosi cha timu hiyo hata hivyo ameshisha Ligi ya Spain La liga,ameshinda mashindano ya Ulaya,na kacheza klabu bingwa nusu fainali,lakini huyu anaonekana anathamani ndogo kuliko kinda la hapa uingereza,katika  wastani  wetu wa malipo ya mshahara  yeye ndio sahihi kwetu ’’alisema Mourinho.

1 comment: