MATUKIO ya ukatili wa kijinsia ni
moja ya mambo yanayorudisha nyuma harakati za kumkomboa mtoto wa kike katika
ukatili wa kijinsia.
Zipo njia nyingi zinazotumika
kuendesha matukio ya ukatili wa kijnsia ikiwemo ajira za majumbani, ambazo kwa
asilimia kubwa zinaendelea kuchochea suala hilo huku walengwa wakiwa hawajui
sehemu ya kwenda haki zao.
Baadhi ya watu katika jamii ambao
wamekuwa si waaminifu wamekuwa wakiitumia dhana ya ajira za majumbani kuendesha
vitendo vya kijinsia.
Watu hao mara nyingi katika
kutekeleza uovu wao wamekuwa wakienda vijijini na kuchukua wasichana wadogo kwa
kuwarubuni kuwaleta Dar esSalaam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani huku
wakijua si kweli.
“Katika mradi wetu tulibaini kuwa
wapo watu ambao wanakwenda vijijini wanachukua wasichana na kuwaahidi kuwa
wanawaleta kwa ajili ya kazi za ndani, lakini baadaye inakuwa tofauti, kuna
mfano mmoja ambao tumeuona Bagamoyo ambako tunaendesha mradi huu pia, msichana
alichukuliwa kutoka Ludewa kuwa analetwa Dar es Salaam kwa ajili ya kazi za
ndani, lakini baadaye kumbe huyo mtu alikuwa na lengo jingine kichwani mwake.
“Mtu huyo aliyejifanya ni
msamaria mwema kumbe lengo lake alitaka kuishi naye kama mke na mume, binti
yule mdogo mwenye umri wa miaka 16 hakukubali kitendo, siku moja waelimishaji
rika ambao tuliwapa mafunzo maalum walipata taarifa juu ya jambo lile na
walikwenda hadi katika nyumba ya yule mhusika aliyejifanya msamaria mwema na
kumchukua kwa ajili ya kumpatia msaada,” anasema Dk. Makula.
Anasema baada ya kuhojiwa
msichana huyo alieleza jinsi alivyochukuliwa na ahadi aliyopewa lakini
alijikuta Bagamoyo akitakiwa kuwa mke jambo ambalo hakukubaliana nalo.
“baada ya kupata maelezo yake walimsaidia
lakini pia walimpeleka kituo cha polisi
na kufungua jalada na baada ya taarifa zile kumfikia mhusika alikimbia lakini
hadi sasa hivi anatafutwa kwa ajili ya kuchukulia hatua za kisheria,” anasema
Dk Makula.
Anasema kupitia mradi wao wa
kupinga ukatili wa kijinsia na mapambano ya Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi
(GBV/HIV ambao unafanyika katika kata kumi na sita Wilayani Bagamoyo wameweza
kufanikiwa kufanya kazi kwa ukaribu na wanajamii ambako wameweza kuibua matukio
makubwa.
Dk.Makula anasema baada ya
kuwapata wasichana waliokumbana na masuala ya ukatili wa kijinsia huanza
kuwahoji, kufikisha mashauri yao kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na baadaye
Polisi kwa ajili ya kufungua mashitaka.
“Hawa wana mawasiliano jamii
tumewapa elimu ya kutosha kuweza kupata taarifa sahihi kwa kila mtu wanayesikia
amepata matatizo ya ukatili au masuala ya Ukimwi, tunazungumza nao kwanza wajue
njia gani watanatakiwa kuzipitia kuweza kupata haki zao, pili tunawaelekeza
namna ya kufuatia kupata hizo haki na sisi wenyewe tukiwasaidia,tunaendesha
programu hii kwa msaada wa Mfuko wa dharura wa Kimataifa wa kusaidia
mapambano dhidi ya Ukimwi ( RFE).
Anasema wameweza kutoa mafunzo kwa wanamawasiliano jamii
ambao kwa elimu waliyopata wameweza kuleta mabadiliko katika jamii wanayoishi.
“Kumekuwa na mwamko kwamba watu wanaweza kutoa taarifa za
matatizo wanayokumbana nayo katika jamii,sasa hivi wanawake au wasichana
wakifanyiwa masuala ya ukatili wa kijinsia wanakuwa tayari kutoa taarifa
tofauti na mwanzoni, mwako umekuwa mkubwa tofauti na mwanzoni,” anasema
Dk.Makula.
Anasema baadhio ya watu katika jamii wamekuwa si wa kweli
kwani wamekuwa wakiwachukua wasichana vijijini kwa ahadi za kuwapatia kazi za
ndani kitu ambacho si kweli.
“Sasa hivi baada ya elimu kuwafikia vizuri imekuwa rahisi,
kwasababu hawa wasichana wanaofanyia ukatili kwa dhana kwamba wanakuja
kutafutiwa kazi za ndani ni wengi, jamii imekuwa ikibadilisha mbinu kila
wakati, lakini sasa hali inaanza kuabdilika kwamba inapotokea mtu anakumbana na
jambo lile basi wanakwenda kutoa taarifa.
Suala la ukatili wa kijinsia limekuwa likikuwa kila siku
kutokana na kadri jamii inavyobadilisha mfumo wa maisha.
Imekuwa kawaida kwa watu kutumia vigezo vya kutafuta
wafanyakazi wa ndani lakini baadaye wengi hutelekeza katiia maeneo mbalimbali
baadaya kufanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kubakwa na wakati mwingine
kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi.
Jamii kwa kushirikiana na serikali imekuwa ikipigia kelele
suala hili lakini mara nyingi wasichana hao ambao ni wahusika wakuu wamekuwa
hawana taarifa sahihi za wapi waende kutoa taarifa kwa ajili ya kupata msaada
wa kisheria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment