![]() |
Kada wa CCM, Badili Mangula akitoa mada |
Hata hivyo viongozi hao wanatakiwa lazima wawe wametosheka
na wasitawaliwe na tamaa jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi kwa ufasaha
zaidi na kufikia malengo.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa CCM wa jimbo la Kawe,
Badili Mangula alipokuwa akitoa mada ya wajibu na majukumu ya katibu kwa mujibu
wa katiba ya Chama katika semina ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa
Chama na jumuia wa ngazi ya kata katika jimbo la Temeke.
“ wakati umefika kwa viongozi kupewa semina lengo likiwa ni
kuwajengea uwezo na kuwaongezea uelewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa
ufanisi zaidi”alisema Mangula.
Naye mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
ambaye alitoa mada iliyohusu wajibu na majukumu ya mwenyekiti wa CCM kwa mujibu
wa katiba alisema mafunzo ni muhimu kwa kuwa yameelekezwa ndani ya katiba.
“Mafunzo si utashi wa mtu bali yamo ndani ya katiba ya chama
hivyo ni lazima yatolewe kwa viongozu hao ili wawe na weledi wa kufanya kazi ambao utakifanya Chama
kiendelee kushika dola,” alisema.
Kwa upande wake mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu aliwataka
viongozi hao wanaopata mafunzo hayo kuhakikisha wanaenda kuyafundisha kwa
viongozi wa matawi ili nao waweze kuongezewa uelewa.
Alisema semina hiyo ni muhimu kwa viongozi hao kwa sababu
inasaidia kuwapatia mbinu mbadala zitakazowasaidia katika kukipatia chama
ushindi kwenye chaguzi zijazo.
@@@
No comments:
Post a Comment