Monday, 14 July 2014

Kufunga kunasaidia kupunguza unene kwa asilimia kubwa Sehemu 1

Wengi wetu tunaposikia “kufunga”
fikra inayokuja kichwani ni mwezi
Ramadhani na dini ya Kiislamu.
Ukweli hapa Uzunguni ukisema
“unafunga” jambo la kwanza
unaloulizwa ni kama wewe
Mwislamu, kwamba huli nguruwe na
kadhalika. Kinachosahaulika ni
kwamba dini mbalimbali zina tabia
na mtindo wa kufunga na kutokula.
Ila mfungo ninaouongelea si wa
kidini.

Madafu ni kinywaji kizuri sana-
yanaweza kuchukua nafasi ya
vinywaji vya makopo na chupa zenye
sukari na chumvi zisizosaidia mwili.
Kuna watu ambao bado wanasadiki
na kuamini eti madafu husababisha
ugonjwa wa kuvimba miguu au
mbegu za uume! Duu makosa
makubwa maana madafu yanaweza
hata kukinga mambo hayo kwa
madini na protini yake asilia!
Ni mfungo wa kusafisha, kupiga deki
na kukarabati mwili.
Kawaida tunapokwenda haja kubwa
– si kila kitu hutoka. Mabaki tumboni
husongana kule kwa miaka hatimaye
huanza kutuletea vidonda tumboni,
harufu mbaya ya mdomo, ushuzi wa
kutisha, maradhi kama saratani ya
utumbo mkubwa nk. Njia moja ya
kupunguza adha hii ni kutokula kwa
saa 36 kuendelea.

Mboga za majani mabichi ni rutuba
nzuri sana kuondoa unene,
kurutubisha mwili. Hapa majani haya
yametayarishwa na kuwekewa
mafuta ya mbegu iitwayo Kitani
(Flaxseed oil). Unaweza kumwagia
saladi yako mafuta yoyote
yaliyotengenezwa kwa mbegu
mathalan karanga mbichi,
maparachichi, mizeituni, nk.

ITAENDELEA...

No comments:

Post a Comment