
Museveni alisema mwezi Januari kuwa
vikosi vyake vilikuwa vinamsaidia rais Salva Kiir dhidi ya waasi wanaoogozwa na
makamu wake wa zamani Riek Machar. Ushiriki wa vikosi vya Uganda katika mgogoro
wa Sudan Kusini umekosolewa vikali na waasi
Mataifa jirani na ya magharibi, pia
yana wasiwasi kuwa ushiriki huo unazidisha ugumu katika juhudi za kuukomesha
mgogoro huo uliyoibuka miezi saba iliyopita, na ambao unatishia kuitumbukiza
nchi hiyo katika janga la njaa.
Ukurasa mpya wa mahusiano
![]() |
Msemaji wa Riek Machar Miyong Kuon,
alisema mjini Addis Ababa kuwa ujumbe huo wa waasi unalenga kufungua ukurasa
mpya katika uhusiano baina ya waasi hao na Uganda na pia rais Museveni.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni
ya Uganda Fred Opolot hakuweza kutoa maelezo zaidi juu ya ajenda za mkutano
huo, lakini alisema mazungumzo yatajikita juu ya kuondoa mkwamo katika mchakato
wa amani.
Pande hasimu zimefanya mazungumzo
kwa miezi kadhaa mjini Addis Ababa tangu mapigano yalipoibuka katikati mwa
mwezi Desemba, lakini kumekuwepo na maendeleo kidogo sana.
Makubaliano ya kusitisha mapigano
yaliyofikiwa mwezi Januari na Mei yamevunjika. Kiir na Machar pia walikubaliana
mwezi Mei kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, lakini wazo
hilo halijafanyiwa kazi tangu wakati huo.
Alipoulizwa iwapo kuondolewa kwa
vikosi vya Uganda kutajadiliwa na Museveni, afisa wa waasi alisema jambo hilo
ni sehemu ya ujumbe wao, lakini akaongeza kuwa namna, lini na wapi ndiyo mambo
yatakayojadiliwa.
Lakini waziri wa nchi wa masuala ya
kigeni Okello Oryem, alisema suala hilo siyo la kujadiliwa, akiliambia shirika
la habari la reuters kuwa hakuna atakayewamulia lini waondoke Sudan Kusini.
Rais Museveni amekuwa na uhusiano wa
karibu na Kiir, kiongozi wa chama tawala cha SPLA, ambacho kiliongoza mapigano
ya zaidi ya miongo miwili dhidi ya serikali ya mjini Khartoum kabla ya Sudan
Kusini kujipatia uhuru wake mwaka 2011. Nchi hiyo pia ni kituo muhimu cha mauzo
ya nje ya Uganda, na biashara kati ya mataifa hayo iliathiriwa sana na kuibuka
kwa mapigano.
![]() |
Rais Museveni na Salva Kiir. |
Waasi wanyooshewa kidole cha lawama
Wakati huo huo, Marekani imelaani
shambulio la ardhini lililofanywa na waasi dhidi ya wanajeshi wa serikali
katika mji wa kaskazini wa Nassir siku ya Jumapili, na imeonya kuwa Washington
itawawekea vikwazo wale wote wanaokwamisha juhudi za amani.
Umoja wa Mataifa na ujumbe wake
nchini Sudan Kusini UNMISS ulivilaumu vikosi vya Machar kwa ukiukwaji wa
makubaliano ya kusiitsha mapigano.
Licha ya waasi hao kudai kuudhibiti kikamilifu mji huo ambao
ni makao yao makuu ya zamani, Umoja wa Mataifa ulisema mapigano yalikuwa
yanaendelea, huku makabiliano makali zaidi yakiripotiwa jana Jumatatu karibu na
kambi ya wanajeshi wa serikali, magharibi mwa mji huo.
No comments:
Post a Comment