Saturday, 19 July 2014

Wasaidizi watatu waachiliwa huru Darfur



Maafisa wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani Darfur, Sudan, wanasema kuwa wafanya kazi za misaada watatu waliotekwa nyara zaidi ya mwezi uliopita, wameachiliwa huru.
Kikosi cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, UNAMID, walisema kuwa wanaume hao watatu - wote raia wa Sudan - walikuwa mateka wa mwisho kati ya watu 25 waliotekwa nyara mwezi uliopita huko Darfur kaskazini.
Waliobaki wameshaachiliwa huru.
Haijulikani nani aliwateka.
Ni kawaida kwa wafanya kazi wa mashirika ya misaada kukamatwa huko Darfur, eneo ambalo limekumbwa na mizozo katika miaka 11 iliyopit

No comments:

Post a Comment