Staa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametaja sababu zinazomfanya aingie katika
mgogoro na mama yake mzazi, Miriam Sepetu kuwa ni suala la uchumba wake
na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao alikuwa akiupinga mara kwa mara.
Akiongea
na mwandishi, Wema alisema kwa muda mrefu alikuwa akitofautiana kauli
na mama yake katika suala zima la uhusiano wake na Diamond lakini
anamshukuru Mungu amemuelewa na sasa kila kitu kinakwenda sawa.
“Mama
nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini sasa
tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi
nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati
mwanzoni haikuwa hivyo,” alisema Wema huku akiahidi kumkutanisha Diamond na mama yake.
No comments:
Post a Comment