Thursday, 31 July 2014

Kingwendu kuchukua hatua baada ya mkewe KUBAKWA akiwa amelewa

Muigizaji wa filamu za Kiswahili, mchekeshaji Kingwendu yuko katika wakati mgumu baada ya mkewe kubakwa na jirani yake wakati akiwa amelewa pombe.
 
Baada  ya  jitihada  nyingi  za  kumtafuta Kingwendu, hatimaye  mwandishi  alifanikiwa  kumpata  na  kukiri  kuwa  alizipata habari hizo wakati ambapo yuko safarini na majirani walimueleza kilichotokea kuwa mkewe na jirani huyo aliyembaka mida ya saa tano usiku wote walikuwa wamelewa.
 
”Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi juzi, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia.” alisema Kingwendu.

No comments:

Post a Comment