Nyota wa nyimbo za Injili Bongo,
Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu
kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali
mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa,
Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi.Katika ajali hiyo ambayo
Bahati alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili,
dereva wa gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za
usajili IT 7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye
vidole vya miguu na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni
wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake
halikupatikana mara moja.
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari
hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku
akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali,
nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini
kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara
nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi
makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya
kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu
wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni
ya Msama Promotion, Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana
na mwendesha bodaboda.Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho,
kilomita chache kabla ya kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari
lake aina ya Toyota Mark II GX 100.
Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha
bodaboda huyo waliumia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment