Katibu Mkuu wa kamati ya Olympiki ya Tanzania Filbert
Bayi ametangaza kikosi cha wanamichezo 37 na maafisa 10
watakaoiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mjini
Glasgow, Scotland, kuanzia Julai tarehe 23.Tangu michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka wa 2006 Tanzania iliposhinda medali mbili - dhahabu kupitia Samson Ramadhan na shaba ya Fabian Joseph Naali - Tanzania haijashinda medali tena kwenye michezo hii.
Je, mwaka huu unaona Tanzania itazoa dhahabu nyingi zaidi mjini Glasgow? toa maoni yako katika ukurasa wetu wa Facebook:issaadam21@yahoo.com
No comments:
Post a Comment