Klabu ya Schalke imemsajili mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim
Choupo-Moting kutoka kwa hasimu wake wa Bundesliga Mainz. Mkataba wa
nyota huyo katika klabnu ya Mainz ulikamilika mwishoni mwa msimu
uliopita.

Chopo Moting ambaye ni mzaliwa wa Hamburg aliichezea Hamburg SV na kumaliza msimu mmoja katika klabu ya Nuremberg kwa mkopo kabla ya kujiunga na Mainz mwaka wa 2011. Alifunga magoli 20 na kutengeneza mengine saba katika mechi 74 alizochezea Mainz katika Bundesliga.
Aliwahi kuichezea timu ya Ujerumani ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 21 kabla ya kuamua kuichezea timu ya taifa ya Cameroon na akacheza pia katika Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment