
Majaribio ya tiba hiyo yaliyofanywa
kwa waathirika sita wenye virusi vya HIV waliojitolea ni hatua muhimu katika
kile kinachojulikana kama mkakati wa tiba wa "kukitimua na kukiua "
kirusi hicho.
Mbinu hiyo inakusudia kukilazimisha
kirusi hicho cha HIV chenye kudhoofisha uwezo wa mwili kujikinga na maradhi
kutoka ngome yake ya mwisho baada ya kushambuliwa na madawa ya kupunguza makali
ya UKIMWI.
Madawa haya mapya yanaweza kukiweka
kirusi cha HIV katika damu kwa kiwango cha chini cha kuweza kugundulika na
kuwawezesha wagonjwa wenye kuuguwa kurudi kimiujiza katika hali ya maisha ya
kawaida.Lakini madawa hayo inabidi yatumiwe kila siku, yana gharama kubwa na
yana madhara ya pembeni.
Mradi wa majaribio
![]() |
Mkutano wa Kimataifa
wa 20 wa UKIMWI Melbourne, Australia.
|
Iwapo madawa hayo yanasitishwa
kutumiwa kwa kawada virusi vya HIV hurudi tena kwenye kipindi cha wiki chache
na kuanza tena kuziambukiza seli nyengine za kujikinga na maradhi .Kwa hiyo
wanasayansi kwa miaka mitatu iliopita wamekuwa wakielekeza mkakati wao katika
kukitowa kirusi hicho cha HV kwenye ngome yake na baadae kuziua seli zake
zinazojificha.
Katika mhadhara waliouwasilisha
Jumanne (22.07.2014) katika mkutano wa kimataifa wa UKIMWI huko Melbourne
watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Arhus nchini Denmark wameielezea hatua hiyo kuwa
ni kubwa katika mchakato wake wa kwanza.
Wagonjwa sita ambao walikuwa
wakitumia madawa ya kupambana na makali ya ugonjwa wa UKIMWI walitumia madawa
ya kupambana na saratani yanayoitwa romidepsin ambayo yalisababisha uzalishaji
wa seli zilizoambukizwa na kirusi cha HIV kuongezeka kiwango kati ya kipimo cha
2.1 na 3.9 juu ya kiwango cha kawaida.
Kwa wagonjwa watano kiwango cha
virusi vya HIV kilioko kwenye damu kiliongezeka kufikia kiwango cha kuweza
kupimika hatua inayoonekana kuwa muhimu.
Hatua muhimu
![]() |
Nembo ya UKIMWI ya Utepe Mwekundu. |
Mradi huo wa majaribio ulikuwa
ukitaka kujuwa iwapo inawezekana kukichomowa kirusi hicho kinachojibanza na
kukifanya kiweze kuonekana.
Mtafiti mkuu wa mradi huo Ole
Schmeltz Sogaard amesema hii ni hatua kwenye mwelekeo sahihi lakini bado safari
ni refu na kuna vikwazo vingi vya kukiukwa kabla ya kuanza kuzungumzia juu ya
tiba dhidi ya UKIMWI.
Shirika la Kimataifa la Madaktari
Wasiokuwa na Mipaka limesema madawa ya kupambana na UKIMWI bado ni ya ghali ya
mno kwa wagonjwa wengi hususan wale wanaoishi katika nchi zilizoendelea.
Shirika hilo limesema wahanga wa
ugonjwa huo katika nchi za kimaskini hawaathiriki sana na gharama kubwa za
madawa hayo na hutumia kama euro 100 tu kwa mwaka kwa madawa ya kupambana na
ugonjwa huo lakini kampuni za madawa zinawatoza gharama kubwa wagonjwa walioko
kwenye nchi zilizoendelea.
No comments:
Post a Comment