
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia sherehe za Baraza la Idd jijini Dar es Salaam.
Alisema
ingawa hatua za kisheria zinaendelea kwa baadhi ya watuhumiwa
kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi, serikali pia itaweka wazi juu
ya matukio hayo ya mabomu, ikiwemo wanaowatuma.
Alisema
kinachosubiriwa ni kukamatwa watuhumiwa wengine kama wawili, ambapo
aliomba wananchi kushirikiana na Serikali watiwe mbaroni.
“Serikali
haikulala tangu tukio la kurushwa kwa bomu pale Olasiti, tuliongeza
nguvu ya wataalamu wa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na
dalili nzuri zimeanza kuonekana.
“Napongeza
vyombo vya ulinzi na usalama, tumekamata kundi kubwa na baadhi yao
wamekiri kushiriki mambo kadhaa na tutakuja kuwashirikisha,” alisema Pinda.
Alitaka
jamii kufichua watu wote wenye nia ovu ya uhalifu ili wananchi na
jamii nzima iishi kwa amani. Alitaka viongozi wa dini kuepuka mifarakano
ndani ya dini kwa kuwa inasababisha chuki zisizo na msingi.
Alisema
mifarakano ndani ya dini ni mibaya na inapotoka nje na kuwa kati ya
dini moja na dini nyingine, inakuwa mbaya zaidi na kuwasisitizia
viongozi wa dini, kuhakikisha kila dini waumini wanakuwa na amani,
utulivu na mshikamano.
Pinda
alisema anaamini amani na utulivu wa Tanzania, msingi wake ni
mafundisho ya dini. Alisisitiza taifa lolote ambalo halina msingi huo wa
dini, watu wake hawana tofauti na wanyama , kwa kuwa hawana hofu ya
Mungu na hivyo hawaogopi lolote.
Alipongeza
viongozi wa dini wa Dar es Salaam kwa kuunda Kamati ya Amani,
inayohusisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo ambayo hukutana
na kujadili namna ya kuboresha amani bila kujali tofauti zao.
Kutokana
na ubunifu huo wa viongozi wa Dar es Salaam, Pinda alisema kila mkoa
anaokwenda, amekuwa akiwahamasisha wakuu wa mikoa kusaidia kuandaa
kamati kama hizo kwa kuwa ni msingi wa amani.
Baraza
la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) wilayani Arumeru, limeahidi
kushirikiana na polisi mkoani kuhakikisha linafichua watu ambao
wamekuwa wakijihusisha na uvunjifu wa amani mkoani Arusha.
Kiongozi
wa Baraza la Wazee, Wilaya ya Arumeru, Shehe Haruna Husein alisema
hayo jana akizungumza na waandishi wa habari kulaani vikali vitendo
mbalimbali vya uhalifu vinavyoendelea mkoani humo.
Alisema, “Bakwata wilayani Arumeru inalaani vikali vitendo hivyo vya uhalifu vinavyoendelea mkoani hapa.” Alisisitiza watashirikiana na polisi kufichua wahilifu.
Alipongeza
Polisi kwa jitihada zao kudhibiti uhalifu. Alitoa mwito kwa wahisani
wengine kuhakikisha wanashirikiana na jeshi hilo kuwezesha wahalifu
wakamatwe.
“Kwa
kweli sisi kama Bakwata tunalaani vikali sana hivi vitendo vya uhalifu
vinavyoendelea mkoani hapa, huku tukiahidi kushirikiana na jeshi la
polisi katika kudhibiti matukio ya uhalifu yanayoendelea mkoani hapa ili
wahalifu wote wanaojihusisha na matukio hayo wachukuliwe hatua kali za
kisheria,” alisema.
Miongoni
mwa matukio ya ulipuaji mabomu ni pamoja na kwenye Kanisa Katoliki,
Parokia ya Joseph Mfanyakazi, Olasiti. Katika tukio hilo, watu wawili
walipoteza maisha na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Tukio
lingine la ulipuaji bomu, ni kwenye mkutano wa wa Kampeni za uchaguzi
mdogo wa Madiwani wa Chadema katika eneo la Soweto, ambalo pia watu
kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Hivi
karibuni, mlipuko mwingine ulitokea katika mgahawa wa Vama Traditional
Indian Cuisine na kusababisha majeruhi. Baadhi ya watu wanaodaiwa
kuhusika katika ulipuaji wameshafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment