Timu ya taifa ya Tanzania
Kituo cha Kimataifa cha Ulinzi wa michezo (International
Centre for Sport Security) wiki hii kitatoa elimu kuhusu kupiga vita upangaji
wa matokeo kwa wanamichezo vijana wa kiafrika.

Taarifa
zaidi
- michezo
Warsha hiyo ina lengo la kufundisha wanamichezo vijana wenye
umri kati ya miaka 12 hadi 18 wanaotoka katika vyuo vya michezo pamoja na
watoto wa Tanzania wanaoishi maeneo hatarishi.
Warsha hiyo itaanza kwa kuwafundisha wachezaji wa timu ya
taifa ya Tanzania walio chini ya Umri wa miaka 17 katika uwanja Karume mjini
Dar es Salaam nchini Tanzania.
Wachezaji watakaohudhuria semina hiyo watajifunza mada mbali
mbali ikiwemo namna ya kuzuia kupanga matokeo na kuinua vipaji vya wachezaji
vijana, mbinu za kubaini, kuzuia na kuripoti mpango hiyo na namna ya kuonya
kuhusu mipango hiyo hatari ya kupanga matokeo.
Stuart Page wa Kituo hicho cha Kimataifa anasema "
Elimu na Kinga ndio msingi wa Kituo hicho kuondoa matatizo ya upangaji wa
matokeo na hasa wanariadha ndio msingi wa mkakati wa kituo hicho."
No comments:
Post a Comment