
Takriban watu 300 wamepoteza maisha yao thuluthi mbili ikiwa ni raia wa Uholanzi.
Waziri mkuu nchini Uholanzi Mark Rutte amesema kwamba amemwambia rais wa Urusi Vladmir Putin,kwamba ana fursa ya mwisho kuonyesha kwamba anataka kusaidia.
Urusi imeyashtumu mataifa ya magharibi kwa kuzua habari za uvumi dhidi yake.
Urusi imesema kuwa maswali zaidi yanafaa kuulizwa kuhusu mfumo wa ulinzi wa anga ya Ukraine.
Hatma ya kisanduku cheusi kinacho rekodi yanayojiri katika ndege hiyo haijulikani huku viongozi wa waasi wakisema kuwa hakipatikani.
No comments:
Post a Comment