Monday, 14 July 2014

Mwinyi, Mkapa, Jakaya kutunukiwa tuzo Agosti 30

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kupewa tuzo na Kituo cha Michezo cha Sinza cha jijini Dar es Salaam (SSSCC), katika kumbua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
Mbali ya Kikwete, wengine watakaopewa tuzo katika hafla hiyo ya Agosti 30, ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Tatu; Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na wengineo kutokana na mchango wao.
Tuzo hizo zilizondaliwa na kituo hicho kwa kushirikiana na Chama cha michezo, Utamaduni na Sanaa kwa Watanzania Wote (TAFISA), zitafanyika siku katika Hotel ya Delux Sinza.


Kwa mujibu wa Mratibu wa hafla hiyo, Kadatta Kaswella, alisema lengo ni kuwapongeza viongozi hao kama ishara ya kutambua juhudi zao katika maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Viongozi wengine katika tuzo hizo ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuri, Waziri wa Aridhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Pfof Anna Tibaijuka.
Wengine ni Juma Nkamia (Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Kassim Ally Mtawa (Msaidizi Mahususi wa Rais), IGP Evarist Mangu (Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania) na Abdulrahman Kaniki (Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi).
Kuhusu Mkapa, alisema ni jitihada zake za kuwaachia Watanzania Uwanja wa Taifa ambao unalisaidia Taifa katika mashindano  huku Waziri Nkamia akipongezwa kwa kuteuliwa kwake, hivyo ni busara kuwapongeza watu wakiwa hai.


Aliongeza, siku hiyo ya hafla mgeni rasmi atakuwa Waziri Dk. Mwankyembe huku hafla hiyo ikipambwa na burudani murua.

No comments:

Post a Comment