
Makombora matatu yaliyofyatuliwa kutoka Ukanda wa Gaza yamepiga kusini mwa
Israel, ikiwa ni saa mbili tu baada ya makubaliano ya kusitisha mashambulizi
kuanza kutekelezwa. Jeshi la Israel limesema makombora hayo yalianguka katika
eneo la Eshkol, ambalo liko katika mpaka wa Kusini mwa Ukanda wa Gaza. Hamas
imekanusha kuhusika kwa vyovyote na shambulizi hilo. Ihab Ghusein, mkuu wa
habari wa serikali ya zamani ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, imesema
makubaliano ya kuweka chini silaha yalikiukwa na Israel ambayo ilitumia vifaru
kufanya mashambulizi wakati wa kipindi hicho. Jeshi la Israel baadaye lilisema
mlipuko karibu na mpaka ulimjeruhi mwanajeshi mmoja, bila kutoa maelezo zaidi.
Jeshi lilijibu kwa kufyatua makombora. Mashambulizi hayo yalivuruga mpango wa
kuweka chini silaha uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa misingi ya kibinaadamu,
ambao Israel na Hamas walikubali kuutekeleza kwa muda wa saa tano hapo jana.
No comments:
Post a Comment