Friday, 1 August 2014

Taarifa za usajili:Man United wapigwa bao na PSG kwa Angel Di Maria





Kwa mujibu wa taarifa  kutoka BE IN SPORT katika mtandao unaomilikiwa na Qatari pia wamiliki wa klabu hiyo(PSG) inayocheza ligi kuu ya Ufaransa zinasema kuwa tayari klabu mbili zimeshakubaliana kimsingi kwa mkopo wa pouni 8m ambayo watakuwa wakimuhudumia kila kwa msimu ujao. 
Hata hivyo ili dili hiyo iweze kufanya kazi katika usawa wa kimichezo PSG watalazimika k numuuza mchezaji mwenye jina kubwa klabuni hapo kuendana na sheria inavyowataka kufanya.
Man United wanamatumaini ya kumchukua ambaye walikuwa wakimsaka kwa muda mrefu (Edinson Cavani),ingawa mchezaji huyo kutoka taifa la Uruguay anafuraha kumuona Di Maria akijiunga na mabingwa hao wa ligi 1.

Kuhusu Louis van Gaal
"Muda wato tunaangalia mchezaji anayefaa kuungana katika kikosi chetu,” Van Gaal akiongea na mtandao wa L'Equipe ulioko Ufaransa.
Van Gaal alisema"Angel di Maria ni mchezaji mwenye hadhi ya kimataifa na mwenye kipaji,Tuna mkaribisha katika kikosi chetu."

No comments:

Post a Comment