
Kwa
mujibu wa wananchi walishuhudia tukio hilo wamesema wameshuhudia kundi
la madereva wa pikipiki wakimshusha mtu huyo kisha kummwagia mafuta ya
taa na kumchoma moto ambapo wameomba jeshi la polisi kufuatilia tukio
hilo walohusika wachukuliwe hatua.
Wananchi
wakazi wa kata ya mkundi wamesema hilo sio tukio la kwanza kutokea
kwa watu kuuwawa na kisha kuchomwa moto na kuomba vyomba vya sheria
kufanya kazi zake kwani huenda matukio hayo yanatokana na watu kuchoshwa
na baadhi ya matukio ya wizi ambayo watuhumiwa huachiwa huru na vyombo
vya sheria pasipo kuchukuliwa hatua.
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo .
No comments:
Post a Comment