Thursday, 7 August 2014

NEVILLE kutoendelea tena na kazi ya ukocha, Manchester United

Neville alitambulishwa rasmi kufanya kazi ya uchambuzi kwenye TV wakati wa kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil. PHILI Neville amepiga chini kazi ya ukocha chini ya Louis Van Gaal katika klabu ya Manchester United na msimu ujao atakaa kwenye sofa za TV kuchambua mechi.Baada ya kutangazwa kuwa miongoni mwa watu wanaounda timu ya  MOTD katika harakati zake za kutimiza miaka 50 ya kutangaza ligi, Neville aliwaambia wafuasi wake milioni moja kwenye mtandao wa Twita kuwa hataendelea tena na kazi ya ukocha Manchester United ambapo alifanya kazi kama kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza chini ya David Moyes msimu uliopita.



No comments:

Post a Comment