Habari
za kuaminika zinadai kwamba tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha
tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la
Mwengi Ally.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi
alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili
lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.
Ilidaiwa
kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka
wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua
kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake,
angeumizwa Aunt alikimbilia nyumbani kwa shoga yake, Wema.
Ilidaiwa
kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi
wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na
meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye
walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na
waume za watu.
Ilisemekana
kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake
aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao
kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani
yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe
akanasa meseji zao za mapenzi.
Baada
ya kujazwa data hizo, Mwandishi alimtafuta Mwengi ili kupata maelezo ya
kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema
lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa
yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya
Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.
Alisema
baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama
yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond,
kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi
nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake,
nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.
“Nilipoisoma
ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi
yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake
nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa
jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,” alisema Mwengi.
Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”
No comments:
Post a Comment