Thursday, 7 August 2014

Wenger kutest vifaa vipya katika mechi ya jumapili dhidi ya Man city



Jumapili iliyopita  Gunners waliweza kuwachezesha wachezaji wao wapya na kuambulia kipigo cha  1-0 dhidi ya Monaco katika kombe lao la Emarate cup .
 kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema kuwa anategemea kuchezesha kikosi ambacho kitaleta ushindani katika mechi ya juma pili ambapo watakutana na Man City katika uwanja wa Wembley wachezaji wa Arsenal wanao tegemewa kuwanza ikiwa ni pamoja na  Sanchez (£35m), Debuchy (£12m) na (Chambers £16m).
Alipoulizwa kama anampango wa kuchezesha kikosi ambacho kilicheza na Monaco jumapili iliyopita Wenger alisema”Ndio ikiwezekana kuwachezesha watacheza”.
.
Katika maandalizi ya jumapili na  Manchester City
“Bado hatupo tayari , physically, lakini tutakuwa vizuri zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Monaco.Hata hivyo ni jaribio zuri kucheza na  Man City, kwa kuwa wao ni mabingwa wa msimu uliopita”alisema wenger na kuongeza kuwa hana uwakika kama David Ospina ataweza kucheza mechi hiyo kutokana na kutokuwepo mechi iliyopita.

No comments:

Post a Comment