Tuesday, 12 August 2014

Waziri muhongo awataka watanzania kuchangamkiai fursa zinazotolewa na China




Wizara  ya Nishati na Madini  imetoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo zinazotolewa na china ili kuweza kutumia elimu hiyo kwa maendeleo endelevu ya sekta za Nishati na Madini.
Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana,Waziri wa Nishati na Madini, professor Sospeter Muhongo alisema nafasi hizi zinapatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Alisema vigezo vinavyo tumika katika  kupata ufadhili ni aina ya kozi aliyoisoma  mwombaji katiaka shahada ya kwanza au uzamili,chuo alicho soma shahada ya kwanza,kiwango  cha  ufaulu  katika shahada ya kwanza kuanzia GPA 3.0 na uwiano wa jinsia.
“Nafasi hizi zinapatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari ambapo vigezo vinavyotumika kupata kupata ufadhili ni aina ya kozi uliyoisoma mwombaji, ”alisema muhongo.
Pia alisema kuwa Serikali ya china imetoa ufadhili  wa nafasi kumi (10) za masomo kwa watanzania katika ngazi ya shahada uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.
Alisema katika shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 walioomba ufadhili ambapo  katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja kati ya wanne walio wasilisha maombi.

No comments:

Post a Comment