Friday, 15 August 2014

Waandishi wa habari wametakiwa kuacha kushirikiana na UKAWA



WAANDISHI wa habari wametakiwa kuacha kushirikiana na Taasisi binafsi na wanasiasa wasiokuwa na nia njema ya kupatikana kwa katiba mpya.
Tahadhari hiyo imetolewa na jana na Balozi wa Amani nchini, Risasi Mwaulanga aliyesema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wenye nia ya kuwapotezea Watanzania fursa ya kupata katiba mpya kwa maslahi yao binafsi.
Akitolea mfano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema kwamba wamekuwa wakitumia vyombo vya habari vibaya kwa nia ya kupoteza fursa ya Watanzania kupata Katiba mpya.
Alitoa wito kwa Ukawa kurejea bungeni kupambana kwa hoja na si kutumia propaganda za kupotosha umma.
“Tangu walipoanza Ukawa wamejipambanua kwa kuonyesha kwamba wapo tofauti na malengo ya kupatikana kwa katiba huku kwa makusudi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kufaanikisha malengo yao,”alisema Mwaulanga.
Alisema kuwa kipindi kilichopita katika bunge maalumu la Katiba Mbowe alishawahi kusema kwamba katiba mpya itapatikana kwa ngumi na mateke sasa cha kushangaza aanakuwa mstari wa mbele kupinga upatikanaji wa katiba hiyo.
“Katika moja ya vikao vya bunge la katiba awamu iliyopita, Mbowe aliwahi kusema kuwa, ni lazima katiba ipatikane kwa ngumi au mateke. Lakini inashangaza leo kuwa mpingaji naamba mojaa wa kupatikana kwa katiba mpya huku akiwa anatetea maslahi binafsi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment