
Kauli hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine (AFRIMMA) 2014.
Hofu ya kuoa
Akizungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa gazeti maarufu hapa mjini, Diamond alisema kuwa anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho hataki kimtokee maishani mwake.Kumbe!
Jamaa huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, liko Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.
No comments:
Post a Comment