Saturday, 2 August 2014

MONACO:Radamel Falcao haendi popote……..!



Kocha Mkuu wa Monaco Leonardo Jardim ameweka wazi kwamba nyota wake Radamel Falcao hatokwenda  popote.
Akiwa mchezaji mwingine anayetoka Colombia akitakiwa na Madrid baada ya uvumi kuwa kunauwezekano wayeye kumfuata  James Rodriguez aliyoko Real Madrid.
"Katika hatua hii Falcao ni mchezaji wetu na Falcao atakuwa na  sisi kwa asilimia 100 na hatutaki kumwacha," Jardim alisema.
"Ni huruma kumpoteza  James lakini tunaweza kuhesabu juu ya Falcao kuwepo hapa. Bila kujali nini watu wanasema, yeye ni mchezaji wetu. Yupo katika hatua za mwisho kuakikisha anarudi katika kiwango chake na katika msimu huu atakuwa na sisi."
Monaco walimpoteza Rodriguez kwa pouni 63million lakini ili waweze kumudu kuwepo katika nafasi ya kwanza katika ligi ya mabingwa wataitaji kumbakiza star huyo wa Colombia ikumbukwe kuwa Monaco kushiriki ligi ya mabingwa hatua ya makundi kwa miaka tisa.

Falcao alianzia benchi huku Dimitar Berbatov akianza katika uwanja wa Arsenal Emirates siku ya Jumamosi, na Monaco wakaibuka na ushidi wa 2-1 dhidi ya  Valencia  katika kombe la wao Kiarabu Kombe la Emirates Cup tie.

Falcao alikuwa akicheza kwa mara ya kwanza tangu apate maumivu ya kuumia goti Januari na kupelekea kutokushiliki Kombe la Dunia nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment