Idara
ya uhamiaji mkoani Kigoma, imewakamata raia 26 wa Burundi na wawili
kutoka kongo DRC na Rwanda, baada ya kuingia na kuishi nchini kinyume
cha sheria .
Idara hiyo pia imewarejesha raia 11 wa burundi waliomaliza kifungo
baada ya kuhukumiwa mwaka mmoja uliopita kwa makosa ya kuingia nchini
bila vibali.
Afisa uhamiaji mkoa wa kigoma Ambrose Mwanguku amesema raia hao ambao
wamekuwa wakitumia njia zisizo rasmi kuingia nchini wamekamatwa mjini
kigoma pamoja na katika kijiji cha kalinzi, kufuatia oparesheni
inayoendeshwa na maafisa uhamiaji, ambapo amewataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili kufanikisha kampeni ya kuhakikisha
watu wote wanaoishi nchini kinyume cha sheria wanaondoka.
Kwa upande wao baadhi ya raia wa Burundi waliokamatwa wamesema wengi
wa vijana wa Burundi wanaoingia nchini wanakuja kwa lengo la kufanya
kazi za shamba kutokana na hali ngumu ya ajira nchini mwao, huku wengine
wakiwa wameoana na watanzania
No comments:
Post a Comment