Watu
wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuwaua mume na mke na
kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake
aliyeuawa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara
mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.
Kwa
mujibu wa mtoto mkubwa wa marehemu amesema majambazi hao walivamia
nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe
kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio,
Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake
haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment