Hali hiyo, inapelekea wafanya biashara wengi kutokuthamini kuweko
kwa jengo hilo na kuona halina msaada kwao,
kutokana na madai ya kuwepo kwa mapungufu makubwa katika maeneo ya jengo hilo ikiwa
ni pamoja na kuwepo kwa miundo mbinu mibovu, kukosekana kwa lift na kutokuweko
kwa kituo cha mabasi ambacho kitasaidia kuwepo kwa wateja wanao toka maeneo mbalimbali
jijini.
Mwenyekiti wa wanyabiashara katika jengo hilo,
Abubakari Rakesh, anasema jengo limekosa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ustawi
wa wanyabiashara na kukosekana kwa kituo
cha mabasi ambacho kingekuwa chachu ya kupatikana kwa wateja.
“Miundombinu ya jengo si mizuri kwa kukosa vitu
muhimu kama vile lift,kituo cha mabasi na mazingira mazuri ya kufanyia biashara
ndio maana utaona wafanyabiashara wengi bado wapo soko la Karume kwakuwa pale
kuna kituo cha mabasi na kuna wateja wengi kwa hiyo ni vigumu kuwashawishi kuja
eneo amabalo kwao halina tija,” anafafanua Rakeshi
Rakeshi anasema hali hiyo imepelekea kuwaomba halmashauri
ya jiji na manispaa ya Ilala iwasaidie katika kutatua kero hizo za muda mrefu kwa
kuwa wao ndio wenye dhamana ya jengo lakini mpaka sasa hawajaonesha nia ya
dhati katika kutatua madai hayo ambayo yanatoka kwa wafanyabiashara.
Anasema mpaka sasa ni asilimia 30 ambazo zinaonesha
muelekeo wa mafanikio ya jengo toka limekabidhiwa kwa mamlaka husika japo kuwa
tunapiga hatua katika kushawishi lakini bado zinatakiwa jitihada za makusudi katika
kuhakikisha madai ya wafanyabiashara yana sikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa
kina.
Katika kukikisha wanatafuta ufumbuzi wa
changamoto zinazopatikana katika jengo hilo, Rakesh anasema Agosti 31 mwaka
jana walikutana na kamati ya (MILADI TAMISEMI) Dodoma,chini ya Mwenyekiti Dk Hamisi Kigwangala.
“Katika kueleza kamati matatizo yanayotukabili
ikiwa pamoja na jengo kukosa lift , kituo cha mabasi,na uwepo kituo cha kuoshea
magari mbele ya jengo licha ya kupelekea usumbufu kwa wateja pia inachangia muonekano
mbaya wa jengo, bado mpaka sasa hakuna matokeo yeyote kutoka katika kamati hiyo
ambayo yangetoa ufumbuzi, japokuwa walituahidi wangetupatia ufumbuzi wa suala
hilo mapema,” alisema Rakeshi.
Naye Mwenyekiti Msaidizi, Gerald B.Mpagama,anasema
madai ya wafanyabiashara yanagusa maslahi binafsi ya viongozi walio pewa
dhamana,inapelekea madai hayo yenye
msingi kutosikilizwa na kutatuliwa na viongozi hao jambo ambalo
linadhohofisha makusudio na malengo ya
serikali katika kufanikisha kuwepo kwa jengo hilo.
“Viongozi wa Halmashauri ya jiji na Manispaa ya
Ilala kutokana na maslahi yao binafsi wamekuwa chanzo cha kuwako kwa matatizo
haya kwa muda mrefu na kupelekea kudhoofisha kupatikana kwa ufumbuzi wa matatizo wakati wakijua fika kuwa kuna hasara
kubwa inayo patikana kutokana na malengo na makusudio ya kuwepo kwa jengo kutotimia
kama ilivyotarajiwa ,”anasema Mpagama.
Mpagama anasema kimsingi Rais Kikwete alitimiza
ahadi yake na kulikabidhi jengo tangu 2009, muda wote huo mamlaka husika
wameshindwa kusimamia majukumu yao na kusababisha hasara kubwa kutokana na
wafanyabiashara wengi bado hawaja shawishika kutokana na kutokuwepo na
miundombinu itakayo wavutia wateja.
“Hii sio (mall) kama Mlimani city, kama
viongozi wanashindwa kufahamu kuwa pesa nyingi zimetumika kujenga jengo hili na
mpaka sasa malengo hayajafikia hata robo,wao baada ya kutatua matatizo hili
tufikie malengo,wanadharau na kufikilia ubinafsi na ukiangalia kwa kina Meya wa
manispaa ya Ilala (Jeri Slaa) ndio hajafanya
lolote na kashindwa kusimamia kazi yake kwa maslahi ya umma,badala yake
yeye anaendeleza maslahi binafsi, ”alilalamika Mpagama.
Anasema zipo baadhi ya changamoto zinazo tokana
na utoro wa wanyabiashara ambao wanakuwa na vizimba ambavyo hawafanyii biashara
bado tunaendelea kufanyia kazi na katika kukabiliana na hilo tumeamua kuchukua
vizimba vyote kwa wafanyabiashara wote wasio na sifa na kuwapa wengine ambao
wenye sifa tunazo taka.
“kufungwa kwa vizimba vingi inasababiswa na
kuwepo kwa utoro na kupoteza sifa kwa wafanyabiashara wengi wenye vizimba, kutokana
na hali hiyo tumeamua kuchukua vizimba
vyote kwa wafanyabiashara walio poteza sifa na wasiokuwa tayari katika
maendeleo ya jengo hili ili tuwapatie
wenye sifa za kufanya biashara, ”anafafanua Mpagama.
Katika jitihada za kumtafuta Meya wa jiji la
Dar es salaam, Didas Masabuli, ili kujua kwamba ni namna gani ameweza kutafuta
ufumbuzi wa tatizo hilo la muda mrefu, Meya
wa jiji alidai kuwa hajui madai hayo na kuelekeza labda mkurugenzi wa jiji
angeweza kutambua madai hayo.
“Ningeshauri atafutwe Mgurugenzi wa jiji labda yeye ndio mwenye data kamili ambazo
zitamuezesha kuongelea suala hilo kwa kina,lakini mimi siwezi kuliongelea hilo kwa
kuwa hawaku leta madai yao kwangu , hata
hivyo madai yao siyatambui ndio maana nimeshauri atafutwe mkurugenzi wa jiji ili aliongelee suala
hilo, ”anasema Masabuli.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa jiji naye alimtaka
mwandishi kumtafuta kiongozi wa jengo kwa kuwa hayuko tayari kulizungumzia
suala hilo.
Katika kikao cha kamati (MILADI TAMISEMI),
ambacho kilikuwa chini ya mwenyekiti Dk Hamisi kigwangala na waziri Hawa Ghasia,
kilichofanyika Agosti 31 mwaka jana mjini Dodoma, kwa mujibu wa mwenyekiti wa
wanyabiashara wa Machinga complex
kinaonyesha kuwa baadhi ya viongozi waliokuwepo pamoja na Meya wa jiji la Dar es salaam Didas Masabuli.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Rakesh, katika kikao na
kamati hiyo alipata nafasi ya kuelezea madai
yao mbele ya kamati hiyo pia wakiwemo viongozi
wa jiji na kudai kwamba wange ya shuhulikia madai hayo lakini mpaka sasa
hapaja kuwapo matokeo yeyote amabayo yangekuwa ni matokeo mazuri ya kikao
hicho.
“Nasikitika sana kwa Meya wa jiji anaposema
hayatambui madai yetu, katika kikao ambacho tulikutana na kamati ya (MILADI
TAMISEMI) Dodoma,chini ya mwenyekiti Dk
Hamisi Kigwangala, tukieleza madai yetu nayeye (Didas Masabuli), alikuwapo
kwenye kikao hicho,na haya madai yapo
kwa kipindi cha miaka sita sasa,sidhani kama kuna kiongozi mwenye dhamana na
hili jengo anaweza kusema hajui madai ya wafanya biashara kama anavyodai yeye
(Masaburi), kwamba hayajui madai yetu, ” anasema Rakesh.
Ikumbukwe
kwamba jengo hilo lilijengwa kwa mkopo wa NSSF na likakabidhiwa kwa viongozi wa
Halmashauri ya jiji na manispaa ya Ilala
miaka sita iliyopita lakini mpaka sasa shughuli katika jengo hilo
No comments:
Post a Comment