Monday, 4 August 2014

EXCLUSIVE: Chris Brown akana kutemwa na Karrueche .......!!!!!!!!!!!!




Kutokana na tetesi kwamba Chris Brown katemwa na aliyekuwa mpenzi wake Karrueche, madai hayo ameyakanusha na kusema kuwa yeye ndiye aliye mtema kimwana huyo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo vipo karibu na wapenzi hao zinasema kuwa  Chris alishtushwa na habari zilikuwa kuwa zimeenea kwamba yeye kuachwa na Karrueche badala yeye kumuacha.

Taarifa hizo zilipo takiwa kutaja Sababu zinazodaiwa kuachwa kwa karrueche zinasema kuwa Chris alipogundua Karrueche alikuwa akichati na mwanaume mwingine na kutumiana picha wakati wakiwa pamoja mara.

Taarifa hiyo ilidai kuwa Brown alipatwa na hasira baada ya mwana dada huyo kufanya mahojiano katika maonyesho ya mavazi yake na kuzungumzia juu ya uhusiano wao
Ikumbukwe  Karrueche alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari huko Marekani ivi karibuni akisema kwamba licha ya Chris kuendelea kuwa karibu na Rihhana lakini kinacho muhudhi zaidi ni kwamba bado anavitendo vya kitoto na kuendekeza sana bata na wanawake kuliko shughuli zake za muziki kitu ambacho amekichoka.


No comments:

Post a Comment