Waziri wanchi
ofisi ya Rais sera na uratibu, Steven Wassira anatarajiwa kufunga maonesho ya
tatu ya wanasayansi chipukizi katika ukumbi wa mwalimu Julius Nyerere.
Pia Vijana wametakiwa kuwekeza katika suala
zima la utafiti wa kisayansi ili kuleta maendeleo katika nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana,Kaimu mwenyekiti wa Sayansi chipukizi,Stephen
Nyangonde alisema vijana wanafursa kubwa ya kujiinua kimaendeleo endapo
watajikita kwenye masuala ya kisayansi.
“Kama vijana
watajikita katika masuala ya sayansi watapata kujiinua kimaendeleo kwakuwa kuna
fursa kubwa endapo watakuwa makini,”alisema Nyangonde.
Hata hivyo
Nyangonde aliwataka vijana kutumia
taaluma ya sanaa ili kuhamasisha utafiti wa kisayansi .
No comments:
Post a Comment