CHAMA cha
watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS),kwa kushirikiana na Taasisi za
kutetea haki za binadamu pamoja na jumuia ya watu wenye ulemavu,na shirika la
UNDER THE SAME SAME (USS) wameitaka Serikali kusitisha vibali vya waganga
wa jadi ili kukomesha suala zima la ukataji waviungo vya albino.
Mbali na agizo hili pia wameitaka serikali
kusitisha matangazo ya waganga wa jadi kwa madai kwamba wanapotesha jamii huku
matukio ya ukatili yakiendelea.
Akizungumza
na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa TAS
Gamariel Mboya alisema wamesikitishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa
mtoto wa miaka 15 Upendo Sengerema cha kukatwa Mkono wa kulia wiki iliyopita katika kijiji cha Usinge mkoa wa Tabora.
Alisema
tukio hilo ni la pili kutokea kwa kipindi cha miezi mitatu tangu kuanza kwa
mwaka huu hali inayotishia amani ya kuishi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Kuendelea
kukithiri kwa vitendo hivi vya kikatili
ni ishara tosha kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa uovu huu wa
ukatwaji wa viungo utaendelea huku
walengwa wakubwa wakiwa ni waganga wa kienyeji pamoja na viongozi wan
chi,”alisema Mboya.
Alisema
imekuwa ni kawaida kila ifikapo kipindi cha uchaguzi matukio haya ya kikatili
kuendelea kukua kwani ripoti ya uchunguzi inaonesha kuwa tangu mwaka 2006 mpaka
sasa ni watu 73 waliouwawa ,watu 10 wamekatwa viungo, watu 46 walinusurika
kukatwa na makaburi 18 yalifukuliwa.
Alisema
mpaka sasa watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa jambo
ambalo liawaathiri kisaikolojia na linarudisha nyuma maendeleo.
Alisema
vitendo hivyo vya ukatwaji wa viungo unaonesha ni kwa kiasi gani serikali,wabunge
pamoja na wanasiasa hwana nia ya dhati na utashi wa kisiasa ili kuweka mipango
madhubuti na shirikishi ili kutathmini shughuli za waganga wa jadi.

No comments:
Post a Comment