BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limetakiwa kuendelea
kusimamia uadilifu na kukuza weledi wa
tasnia ya habari nchini kwa kutokana na kutokuwepo kwa sheria yenye kuelekeza
sifa mahususi za mtu anayestahili kuwa mwandishi wa habari.
Pia vyombo vya habari vimetakiwa kuweka utaratibu wa
kutanguliza maslahi ya kitaifazaidi na si ubinafsi kwa sababu kwa sababu
yanaweza kusababisha vurugu.
Hayo yalisemwa juzi na Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Shaban Ally Lila alipokuwa alipokuwa anazindua bodi
mpya ya MCT , alisema hata sheria ya magazeti haina kifungu kinachoweka bayana
sifa ya mtu kuwa mwandishi wa habari hali ambayo inafanya kila mtu kujiona kuwa
anaweza kufanya kazi hiyo, hivyo alishauri kuwe na vigezo vya mtu kuwa
mwanahabari ili kudhibiti makanjanja.
“Heshima ya taaluma hii imekuwa ikichezewa, ni bodi tu ndiyo
pekee ambayo inaweza kurekebisha na kudhibiti wanahabari uchwara, hivyo
natarajia bodi hii mpya itatekeleza wajibu wake kwakiwango cha juu,” alisema.
Jaji kiongozi aliongeza kuwa maadili ya kazi ya uandishi wa
habari huenda sambamba na umuhimu wa stadi za namna ya kutoa taarifa za kweli
ambazo huweza kulikwamua taifa katika majanga mbalimbali, hivyo ni jukumu la
vyombo hivyo kutanguliza maslahi ya
taifa na si ubinafsi.
Pia aliwashauri wahariri kukagua na kujiridhisha kwa taarifa
mbalimbali kabla ya kutolewa katika vyombo vya habari ambapo alitolea mfano katika habari za
mahakama ni jukumu la wanahabari wakisimamiwa a MCT katika uandishi
unaozingatia ufuatiliaji wa karibu wa mashauri yaliyo mahakamani kwa kuonana na
viongozi kupata ufafanuzi wa kesi na kuzingatia nidhamu na kutoegemea upande
wowote wa mwenendo.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo alisema vyombo vya
habari vimekuwa mstari wa mbele katika
kutoa maoni na kuelimisha umma kuhusu ubora na ubovu wa sheria zilizotungwa au
zinazotarajiwa kutungwa, ambapo
vilisaidia sheria mbaya kuachwa kutumika au kurekebishwa pamoja na kutungwa
sheria bora.
Hata hivyo alisema vyombo hivyo katika kutekeleza majukumu
yake katika baadhi ya maeneo na matukio vimeingia kwenye tuhuma na lawama,
ambapo alitolea mfano baadhi ya maeneo yanayolalamikiwa kuwa ni pamoja na kutoa
habari zisizokuwa na ukweli, kuwa na mlengo mmoja, kudhalilisha na kukera,
kutozingatia maadili na weledi.
Pia alisema kuwa kuna
malalamiko kuwa uhuru vyombo vya habari kuwa umeminywa na sheria ya magazeti hasa katika kifungu cha 25 ambacho kinampa
waziri anayehusikka kukifungia chombo cha habari ambacho kwa maoni yake
kinakinzana na mila na maadili ya taifa, ila ni muhimu ikafahamika kuwa hakuna
uhuru usiokuwa na mipaka.
“Kwa nini uogope sheria yenye kutoa adhabu kali iwapo wewe
si mkosaji na wala hutarajii kutenda kosa,” alihoji.
Kwa upande wake Raismstaafu wa MCT, Jaji Dk. Robert
Kisanga alisema miongoni mwa changamoto
zinazoikabili bodi ni pamoja na wamiliki
wa vyombo vya habari kuvitumia kwa
maslahi yao binafsi jambo ambalo si sahihi.
Mbali na wamiliki pia kitendo cha baadhi ya waandishi wa
habari kuandika habari kulingana na matakwa ya wamiliki na si jamii, hivyo
alisema kuna hajja ya kuvinoa ili viweze kufanya kazi zake kulingana na kanuni
za taaluma ya habari.
Wajumbe wapya wa bodi ya MCT ni Rais mpya wa MCT, JJaji
Thomas Mihayo, Hassan Mitawi ambaye ni makamu wa Rais na mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala, Jaji Juxon Mley
ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maadili, Badra Masoud ambaye ni mjumbe wa
kamati ya fedha na utawala na Rose Mwalimu .
Wengine ni Profesa Bernadeta Kilian, Wallec Maugo ambaye
atakuwamjumbe katika kamati zote mbili ya fedha na utawala pamoja na ya
maadili, Ally Mufuruki ambaye atakuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala
na Tuma Ally atakuwa katika kamati ya maadili.
@@@
No comments:
Post a Comment