
Netanyahu alionya kundi la Hamas kuwa
serikali yake itaiadhibu vikali kundi hilo iwapo itathubutu tena
kuidhuru taifa hilo la Kiyahudi.

Kufikia sasa Wapalestina 8,900 wa,rejeruhiwa katika makabiliano hayo .
Israeli inaendeleza kampeini ya kumtafuta
mwanajeshi wake mmoja aliyetekwa nyara na wapiganaji wa Hamas , Hadar
Goldin, Ijumaa iliyopita.
Mwanajeshi wa Isreali aliyetekwa na wapiganaji wa Hamas.
Israel ilianza kuishambulia ukanda wa Gaza
mnamo Julai tarehe 8 ikidai ilikuwa inakusudia kusitisha mashambulizi
ya mara kwa mara ya mizinga na roketi kutoka ukanda wa Gaza.
Hata hivyo Israeli ilianzisha mashmbulizi ya
angani majini na ardhini mara hii ikidai kuwa ilikuwa inalenga kuharibu
njia za chini kwa chini za kundi la Hamas ikidai ndizo zinazotumika
kuishambulia.
No comments:
Post a Comment