Picha za staa wa sinema na Bongo
Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole Kiuno’ zinazomuonesha live akiwa chumbani
tena kitandani kimahaba na mwandani wake, Nuh Mziwanda zimevuja….
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa Shilole, picha
hizo walijipiga wenyewe wakiwa kitandani nyumbani kwa mwanadada huyo,
Kinondoni jijini Dar.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha hizo
walijipiga baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
kwani kabla ya hapo wasingefanya hivyo.
Katika picha hizo zinazowaonesha wawili
hao wakiwa katika mahaba niue, Shilole anaonekana akiwa amemlalia
Mziwanda ambaye naye amejiachia vya kutosha.
Habari za ndani zinadai kwamba mmoja wa
watu wa karibu alishika simu ya Shilole kisha akajifowadia picha hizo
ndiyo chanzo cha kumfikia mtu wetu huyo.
Baada ya kuzidaka picha hizo, mwandishi
alimtafuta Shilole ambaye kwa sasa anakimbiza na ngoma yake mpya ya
Namchukua ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa mashitaka yake
ndipo akafunguka namna alivyochezewa na mtu wa karibu yake.
“Kweli
hizo picha ni zangu na Nuh (Mziwanda), tulijipiga kwa ajili ya
kumbukumbu na tulikuwa na muda mrefu hatujiachia si unajua tena Mwezi
Mtukufu?
“Unajua simu yangu haina
password na nina watu wengi wa karibu so nahisi ndiyo wamezivujisha na
nikimjua namtoa kabisa kwenye network yangu maana siku nyingine anaweza
kunifanyia jambo kubwa baya.”

No comments:
Post a Comment