
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo
umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na
waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza
sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu
amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe
25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua
iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano
hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao
watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze
kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho
tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana
tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano
hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua
nafasi yetu “aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji
wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza
mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha
tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya
kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa
kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu
ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda
kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa
kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi
cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao
kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu
ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa
hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo
tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.
a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu
uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na
wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua
wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.
b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu
ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu
Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu
wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.
c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya
kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva,
Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua
wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha
kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.
d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya
kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki
michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki
mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya
ndani.
e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa
kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika
kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20
kuwa watano tu.
f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars
kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza
wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa
na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.
g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi
ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio
anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake
No comments:
Post a Comment