Monday, 11 August 2014

Maliki kupambana mahakamani, kuulinda wadhifa wake dhidi ya Rais mpya wa Iraq


 
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri Al Maliki anapeleka vita vyake vya kuuulinda wadhifa wake mahakamani, baada ya kutangaza kwamba atachukua hatua za kisheria dhidi ya rais mpya wa nchi hiyo, Fuad Massoum, kwa kukiuka katiba, kutokana na kushindwa kumpa waziri mkuu kutoka kundi kubwa zaidi la wabunge bungeni jukumu la kuunda serikali, mpya.
"Rais fuad Massoum hana haki kuchelewesha uteuzi wa waziri mkuu kutokana na matokeo ya uchaguzi uliopita, hali hii itazidisha matatizo ya kiusalama, ndio maana serikali inakwenda kotini kumshaki rais kwa kukiuka katiba," alisema Maliki.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki.
Hata hivyo mahakama ya juu nchini humo imemuunga mkono Maliki katika harakati zake za kutaka kuiongoza tena nchi hiyo kwa muhula wa tatu.
Vyombo vya habari nchini humo Mahakama hiyo imeamua kwamba kulingana na sheria muungano wa Maliki walio wengi bungeni ndio walio na haki ya kupema jukumu la kuunda serikali, kwa hiyo rais Fouad Massoum atakuwa hana budi ila kumpa Maliki jukumu la kuunda serikali mpya.
Kwa upande wake Marekani inayounga mkono hatua ya rais mpya imesema inatumai Nouri al Maliki hataingilia siasa za nchi hiyo.
Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje John Kerry imesema kuundwa kwa serikali ni hatua muhimu ya kuwepo kwa udhabiti na usalama nchini humo huku akiongeza kwamba kitu wananchi wanachokitaka kwa sasa ni amani kwa hiyo nguvu kupita kiasi hazipaswi kutumiwa na makundi ya kisiasa wakati huu wa kipindi cha demokrasia kwa Iraq

No comments:

Post a Comment