
Kakobe pia alimtupia lawama Rais
Jakaya Kikwete akisema hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo chanzo
cha kuvuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.
Kakobe ametoa kauli hiyo zikiwa
zimepita takriban siku tatu tangu Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya
kila mwezi na kujivua lawama hizo alizokuwa akitupiwa na watu wa kada
mbalimbali.
“Naunga mkono Ukawa si kwa asilimia
100 bali asilimia 150 kwa msimamo wao wa kususia vikao. Tena sitegemei kusikia
wamerejea bungeni, wakirejea watakuwa wamelogwa. Lazima wahakikishe upungufu
huo unafanyiwa kazi kabla ya kurejea kwenye awamu ya pili ya vikao hivyo
vilivyopangwa kuanza Agosti 5,” alisema.
Aliongeza: “Pengine
kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo
ya Tume. Sioni kosa langu ni kutoa maoni kuhusu baadhi ya vipengele vya rasimu
kwa sababu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Mimi kama raia ninayo haki
ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine,” alisema Kikwete kwenye hotuba
hiyo.
Hata hivyo, jana Kakobe
aliyezungumza kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la FGBF alisema kuwa
anapingana na utetezi huo kwani hauna hoja ya msingi kwani alishavuruga
mchakato huo tangu awali.
“Hotuba yake ya kufungua Bunge hilo
ndiyo iliyoharibu mambo yote hadi sasa tumefika katika hali hii.Anafanya hivyo
akiwa na dhamira ya kuvuruga mchakato huo ili usiendelee kwa kuhofia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanguka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Mapendekezo ya wananchi, ambayo yameorodheshwa kwenye rasimu, yanakinzana
na matakwa ya chama hicho hiyo ndiyo sababu,” alisema Kakobe kwa msisitizo.
Askofu huyo alisema, ikibidi Rais
Kikwete angefanya uungwana kwa kurejea tena kwa wananchi kwa kuandaa hotuba
nyingine ili kuwaomba radhi kwa kuvuruga mchakato huo ndiyo mambo mengine
yaendelee.
“Hata kama yeye ni kiongozi, kama
amekosea, anatakiwa kuomba radhi…lazima awatendee wananchi haki yao kwa
kukiri kuwa yeye ndiye chanzo cha mvurugiko huo ili kuruhusu mchakato wa Katiba
uendelee ili Watanzania wapate Katiba wanayoitaka,” alibainisha Askofu Kakobe na kuongeza:
“Sasa umefika wakati wa chama tawala
kukubaliana na mabadiliko yanayotokea. Wananchi wa sasa siyo wale wa zamani
wakuburuzwa tu. Siku hizi watu wajanja, watu wanataka kuona maoni
waliyopendekeza yanafanyiwa kazi bila kuweka usiasa ndani wala si vinginevyo.”
Alisema kuwa juhudi zote za kuunda
kamati kwa ajili ya kufanya vikao vya maridhiano ili kutaka Ukawa warejee
bungeni zimekuwa zikigongwa mwamba kutokana na kukosa uthabiti juu ya hilo.
No comments:
Post a Comment